Kiwanya cha Garden Breeze cha Magomeni jijini Dar es salaam kitajazwa watu siku ya Idd Mosi
Bosi wa African Minofu, Matei Joseph aliiambia sarianews kuwa, anaamini muziki watakaouporomosha utakuwa mkubwa kiasi cha kuchangia kukifanya kiwanja hicho kujaa mashabiki watakaovutwa na burudani yao.
“Binafsi, ni msanii wa siku nyingi ninayefahamu mbinu nyingi za kimuziki, hasa katika kuwavuta mashabiki, hivyo naahidi kukijaza kiwanja hicho kwa muziki mnene zaidi,” amesema Matei.
Matei amesema kuwa, shoo yao ya Idd Mosi katika kiwanja hicho imepangwa kuanza kurindima majira ya saa 12:30 jioni na kuendelea hadi majogoo, ambapo watatumbuiza vibao vyao vipya pamoja na vile vya zamani.
Amesema kuwa pia watarindimisha nyimbo mbalimbali za kukopi kutoka mataifa mbalimbali, huku wakiahidi kuyapa kipaumbele maombi ya mashabiki pamoja na wapenzi wao watakaojitokeza kuhudhuria.
Comments
Post a Comment