Wanaharakati katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na maandishi ya amri 10 za Mungu

Jiwe la amri kumi za Mungu lililoweka mjini Arkansas MarekaniWanaharakati katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na maandishi ya amri 10 za Mungu, kwenye uwanja wa makao makuu ya bunge la jimbo hilo.
Wanasiasa walipitisha kauli ya ujenzi wa mnara huo wa jiwe wenye urefu wa futi sita, katika eneo la Little Rock mnamo mwaka wa 2015.
Muungano wa haki na uhuru wa raia nchini Marekani ACLU, umewasilisha kesi mahakamani kutaka kuondolewa mara moja kwa mnara huo, ukisema kuwa unaleta mgawanyiko na unakiuka ahadi ya uhuru wa kidini kwa wote, katika katiba ya Marekani.
Seneta wa chama tawala cha Republican, Jayson Rapert, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa kutaka kuwekwa kwa jiwe hilo , alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na msimamo wa mahakama kuu ya Marekani, na hivyo ni jambo zuri kwa jimbo la Arkansas.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu