Atimaye Deus Kaseke anatarajia kuongeza mkataba wa miaka miwili kutumikia klabu ya Yanga




KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Deus Kaseke anatarajia kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo iliyobeba ubingwa wa Ligi Kuu bara kwa mara tatu mfululizo.


 Kaseke aliyekuwa likizo kwao Mbeya, alirejea Dar es Salaam kuja kumalizana na uongozi wa Yanga baada ya kuwekewa mezani mkataba wa miaka miwili.


 “Hakuna sehemu yoyote nitakayosaini zaidi ya Yanga ambao nimemalizana nao katika kila kitu muhimu,” alisema kiungo huyo.


 “Yanga ni nyumbani, hizo taarifa za mimi kujiunga na Singida United nazisikia tu lakini ukweli ni kuwa ninasaini Yanga,” aliongeza. Dues Kaseke amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha George Lwandamina tangu alipotua akitokea timu ya Mbeya City.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu