Misri yatoa visiwa vyake kwa Saudi Arabia

Bunge la Misri limehalalisha Saudi Arabia kumiliki visiwa viwili vya nchi hiyo ambavyo havikaliwi na watu.
Mwaka uliopita palitokea maandamano makubwa baada ya serikali ya nchi hiyo kusema kuwa itatoa visiwa hivyo vya Tiran na Sanafir.
Mahakama kuu nchini Misri ilipinga jambo hilo lakini serikali ikasema ni suala ambalo lipo ndani ya uwezo wa serikali.
Sasa idhini ya mwisho inahitaji kutolewa na Rais Abdul Fattah al-Sisi
Waandamanaji walikusanyika nje ya makaa ya chama cha habari mjini Cairo wakati taarifa zilipoibuka juu ya hatua hiyo ya bunge. Watu kadha wakiwemo waandishi wa habari walikamatwa.
Rais Sisi alisema kuwa wakati wote visiwa hivyo vilimilikiwa na Saudi Arabia na kwamba Saudi Arabia, ilikuwa imeomba misri kuweka vikosi vyake huko mwaka 1950 ili kuvilinda.
Mwezi Januari mahakama ilisema kuwa serikali ilikuwa imeshindwa kutoa ushahidi kuwa visiwa hivuo vilikwa ni vya Saudi Arabia, licha ya hakumu hiyo kubatilishwa na mahaka nyingine miizi michahe baadaye.
Wapinzani wanamlaumu Bwana Sisi kwa kukiuka katiba na kusalimisha visiwa hivyo kwa Saudi Arabia, nchi iliyomuunga mkono kifedha tangu aongoze mapinduzi ya kijeshi kumundoa madarakani rais aliyechagulia Mohamed Morsi mwaka 2013.
Visiwa vya Sanafir na Tiran:
  • Sanafir na Tiran ni visiwa ambayo viko umbali wa kilomita 5 kutoka kingine katika bahari ya Shamu.
  • Tiran kiko Ghuba ya Aqaba katika eneo muhimu ambalo Israel hutumi kuingia bahari ya Shamu
  • Visiwa hivyo havina watu, isipokuwa vikosi vya jeshi la Misri na vingine vya kulinga amani.
  • Wanajeshi wa Misri wamekuwa kwenye visiwa hivyo tangu mwaka 1950 kupitia ombi la Saudi Arabia.
  • Israel ilitenka visiwa hivyo mwaka 1956 na 1967 mtawalia na kuvirejesha kwa Misri kwa pamoja.
  • Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi alilaumiwa kwa kuuza ardhi ya Misri baada ya kuamua mwezi Aprili mwaka 2016, kusamisha visiwa hivyo kwa Saudi Arabia.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu