KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano (Messi) amemuwahi mwenzake Simon Msuva baada ya kuondoka nchini juzi kujiunga na klabu ya Difaa Hassan D’Eljadida iliyoshiriki ligi kuu nchini Morocco. Messi ambaye mkataba wake umemalizika hivi karibuni na klabu yake ya Azam amekwenda nchini Morocco kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo yenye timu 16. Wakati Messi akiondoka nchini humo winga wa Yanga, Simon Msuva ambaye naye anapigiwa hesabu na klabu hiyo anatarajia kuondoka nchini alhamisi hii ili kujiunga na klabu hiyo. Meneja wa Azam, Philp Alando alipoulizwa kuhusu safari ya winga huyo alisema kuwa klabu hiyo aina taarifa na lolote lile kwa kuwa walimalizana naye toka mkataba wake umemalizika. “Mkataba wa Singano ulikuwa umemalizika Julai 8 mwaka huu hivyo sisi hatuna mazungumzo naye yoyote na wala hatujui kuhusu safari hiyo ya Morocco wala chochote kinachoendelea,” alisema. Wakati ...
Popular posts from this blog
Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger
Arsene Wenger amemuorodhesha winga wa Manchester United Anthony Martial katika orodha yake ya washambuliaji anaotaka kuwanunua kiangazi hiki. Kocha huyo wa Arsenal ameanza kumkatia tamaa kinda wa Monaco Kylian Mbappe na sasa anampigia hesabu Martial. Wenger anajiandaa kulipa pauni milioni 40 kwa Martial, ambaye amekosa nafasi ya kudumu Old Trafford chini ya Jose Mourinho. Hata hivyo Wenger anahofia kuwa Mourinho anaweza kumbania kutokana na uhasimu mkubwa ulioko kati yake na kocha huyo wa Manchester United.
Makaburi kumi yagundurika katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo katika mkowa wa kasai
Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema kwamba imepata zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa Kasai, mahali ambapo vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia. Mwendesha mastaka wa kijeshi Generali Joseph Ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa Kamuina Nsapu ambao wamekuwa wakipiga vita majeshi ya serikali. UN yathibitisha makaburi ya pamoja DRC Zaidi ya watu 500 wauawa DRC tokea mwezi Machi Zaidi ya watu 3000 wameuwawa DRC tangu Oktoba Mnamo wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea kila uchao katika mkoa huo, ambapo takriban watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu. Umoja huo aidha ulinyooshea kidole jeshi la taifa la Kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu. Hata hivyo jopo maalum la uchunguzi wa mauaji hayo iliamua kwamba hakuna uhalifu wowote wa kivitu uliyotekelezwa na kwamba hakuna mapigano yaliyotangazwa rasmi mkoani Kasa...



























Comments
Post a Comment