Aliyempiga mbunge wa Republican risasi auawa Marekani

Mtu mwenye silaha ambaye aliwafyatulia risasi wabunge wa Republican wakati wakifanya mazoezi ya mchezo wa baseball mjini Washington DC ameuwa.
Kinara wa walio wengi bungeni Steve Scalise, ni mmoja wa wale waliojeruhiwa wakati wa kisa hicho cha mapema asubuhi katika hustani huko Alexandria , Virginia.
Mshambualiaji ambaye ni mzaliwa wa Illiois James T Hodgkinson, mwenye umri wa miaka 66, aliuawa baada ya ufyatulianaji wa risasi na polisi.
Waliojeruhiwa ni pamoja na polisi wawili.
Hodgkinson alikuwa amemfanyia kampeni mgombea urais wa Democratic Bernie Sanders.
Ukurasa wa Facebook ambao unaonekana kuwa wa Bwana Hodgkinsion, umejaa propaganda dhidi ya Republican na Trump.
Bwana Sanders ambaye ni Seneta wa Vermont amesema amehusunishwa na kitendo hicho cha Hodgkinson.
Rais wa Marekani Donald Trump ametaja shambulia hilo kuwa la kinyama.
Trump alimtembelea bwana Scalise ambaye alipiwa risasi kwenye nyonga na yuko hali mahuti baada ya kufanyiwa upasuaji.
Hospitali ilisema kuwa Bwana Scalise alivunjika mifupa, na kupata majeraha ya viungo vya ndani na hivyo atahitaji upasuaji zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu