Wakiwa wanaelekea kuwa wachezaji 'pacha' ghali zaidi katika Premier League - Romelu Lukaku na Paul Pogba wanajifua vilivyo kwenye likizo yao huko Marekani.
Jose Mourinho anaamini kuwa klabu yake imefikia makubaliano na Everton ya kumnunua Lukaku kwa pauni milioni 75 ambayo itamfanya awe mchezaji ghali wa pili katika Premier League nyuma ya Paul Pogba aliyenunuliwa kwa pauni milioni 89.
Wawili hao wenye urafiki wa hali ya juu, wako mapumzikoni Los Angeles na wamekuwa wakijifua pamoja tayari kwa msimu mpya.
Lukaku anategemewa kufanya vipimo vya afya huko huko Los Angeles na inaaminika kuwa dili hilo lina ushawishi mkubwa kutoka kwa Pogba.
Maswahiba Romelu Lukaku na Paul Pogba wakijifua kinoma
Comments
Post a Comment