Hatimaye kwa siku ya jana timu ya EVERTON YALETA RAHA UWANJA WA TAIFA ...Rooney 'aiteka' Tanzania Gor Mahia ikilala 2-1






Akiwa katika ardhi ya Tanzania ndani ya dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Wayne Rooney akaifungia Everton bao lake la kwanza tangu arejee timu hiyo akitokea Manchester United.


 Katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, Rooney akaufanya uwanja wa Taifa ulipuke kwa furaha pale alipoifungia Everton bao la kwanza kwa shuti la mita 30 kunako dakika ya ya 37.


 Katika mchezo huo ulioisha kwa Everton kuibuka na ushindi wa 2-1, ikawachukua Gor Mahia dakika mbili tu kusawazisha bao kupitia kwa Tuyisenge. Wakati mchezo ukielekea ukingoni, Everton wakapata bao la ushindi dakika ya 86 kwa mkwaju mkali wa Kieran Dowell.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu