Hatimae kocha wa Panone FC jumanne Ntambi amejiunga na mwadui fc kuchukua nafasi ya Ali Bushir






ALIYEKUWA kocha wa Panone FC, Jumanne Ntambi amejiunga na Mwadui FC kuchukua nafasi ya Ali Bushir aliyetupiwa virago. 


Ntambi aliyewahi kuifundisha Mwadui miaka ya nyuma, amesaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao. Katibu mkuu wa Mwadui, Ramadhani Kilao alisema Kocha huyo ataungana na Khalid Adam aliyekuwa kocha msaidizi wa Julio na Bushir. 





Alisema kuwa kati ya makocha hao, baada ya kusaini mkataba wanaangalia nani atakuwa kocha mkuu kwa sababu wote wanalingana kiwango cha elimu ambacho ni leseni ‘B’. “Baada ya kumuondoa Bushir tumemleta kocha mwingine anaitwa Ntambi, anaendelea na mazoezi na timu lakini kesho (juzi), ndio atasaini mkataba ila tutaangalia nani atakuwa kocha mkuu yeye na Khalid,” alisema Kilao.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu