Hatimae simba wiki hii simba yapokea kichapo na timu ya wenyeji wao wa afrika kusini katika kujipima nguvu




VIGOGHO wa Soka Tanzania, Simba SC mapema wiki hii wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu katika kambi yao ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Orlando Pietes. 


Kwa mujibu wa msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon Joseph Omog ilicheza vizuri pamoja na kufungwa.




 “Kwa mujibu wa maelezo ya benchi la ufundi mchezo ulikuwa mzuri na timu ilicheza vizuri lakini bahati ilikuwa kwa wenyeji wao kupata ushindi huo," amesema Manara. Manara amesema Omog anayesaidiwa na Mganda Jackson Mayanja aliwapa nafasi karibu wachezaji wote kucheza akipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu