KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.




KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.



 Hii ni wiki ya pili sasa Simba imepiga kambi nchini Afrika Kusini ikijifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku lengo kubwa kwa kocha wao huyo raia wa Cameroon likiwa ni kutwaa taji ambalo linashikiliwa na mahasimu wao Yanga. Akizungumza kutoka Johannesburg, kocha Omog alisema mechi hiyo ndiyo iliyompa taswira kamili ya ubora wa kikosi chake baada ya kufanya mazoezi magumu kwa muda wote ambao wapo nchini humo.



 “Nimependekeza kucheza na timu hii kwa sababu ndiyo kipimo kizuri kwa mazeozi ambayo tumeyafanya hapa nchini lakini kitu kikubwa kwangu sio kuangalia matokeo bali ninachotaka kuona ni namna gani wachezaji wameyashika yale tuliyoyafundisha na jinsi wanavyoyafanyia kazi,” alisema Omog. Omog alisema kwa maandalizi waliyoyafanya anaamini msimu ujao watakuwa ni moja ya timu inayopigania ubingwa wa Ligi ya Bara na anawashukuru viongozi kwa kuwapa maandalizi mazuri ya sasa kazi imebaki kwao kurudisha shukrani kwa kutwaa mataji yote ambayo wanagombania.




 Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea nchini Agosti 6 na siku mbili baadaye kitashuka kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam kupambana na Rayon Sports ikiwa ni siku maalum kwa timu hiyo (Simba Day), ambayo hufanyika kila mwaka huku dhumuni lake kubwa likiwa ni kutambulisha wachezaji wapya pamoja na jezi.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu