Kusaga aacha ujumbe mzito msiba wa Kibonde ‘vijana tuache nyodo, kama uhai ni pesa basi watu wetu wasinge kufa”
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga ametoa ujumbe mzito katika salamu za Clouds Media wakati wa mazishi wa mfanyakazi wao, Kibonde aliyefariki akiwa mkoani Mwanza akipatiwa matibabu.
” Hakuna msanii Mkubwa na maarufu zaidi ya Ruge wala zaidi ya Kibonde kwa hapa Tanzania. Hakika tuache majivuno ulimbukeni wa mali umaarufu na Madaraka Kwani hivi vyote ni vyakupita na tutaviacha Hapa Hapa Duniani.
Kama UHAI ungekua ni pesa basi watu wetu wasinge kufa maana tungetafuta pesa kwa namna yeyote ili ili ndg zetu wapone. Lakini hakuna Mtu yeyote Duniani mwenye uwezo wa kununua UHAI wala kuzuwia Mauti.
Vijana tupendane sana sana na tuache kujivuna na kujiskia”- Mkurugenzi Mkuu Clouds Media Group’ Joseph Kusaga J Kusaga. RIPkibonde
chanzo BONGO 5
Comments
Post a Comment