Hatimaye timu ya F stars kuiyaidhibu timu ya KIITEC stars ya jijini Arusha kwa magoli 4-2

Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa stars imeibuka na ushindi mzito wa mabao manne kwa mawili (4-2) dhidi ya timu ya chuo cha mawasiliano na kompyuta Kiitec unitedkatika uwanja wa chuo hicho uliopo maeneo ya Moshono jijini Arusha.



Mchezo huo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza kihistoria siku ya Ijumaa ya tarehe 08 February 2019, katika dimba hilo la Moshono na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa timu zote mbili huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo.



Mchezo ulianza kwa kasi ya aina yake huku Fanikiwa Stars wakiongoza kwa kulishambulia kwa kasi lango la timu ya Kiitek United na baada ya dakika chache tu baada ya mpira kuanza, mchezaji wa Fanikiwa Stars alichezewa rafu katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Patrick Tembaakaamuru penati ipigwe na Fanikiwa Stars kuandika bao la kwanza, hadi kipindi cha kwanza kuisha Fanikiwa Stars walikua wakiongoza kwa ushindi wa bao 2-0.



Baada ya mapumziko Kiitek United walikuja kwa kasi wakilisakama lango la Fanikiwa Stars kwa kutafuta nafasi ya kusawazisha, na hatimae dakika ya 54 nahodha wa timu hiyo alipiga mpira wa kutenga uliokwenda moja kwa moja katika lango la Fanikiwa Stars na kuiandikia timu yake bao la kwanza la kusawazisha.



Hadi dakika tisini za mwamuzi wa mchezo huo zinamalizika Fanikiwa Stars walikua wakuongoza kwa magoli manne kwa mawili ya Kiitec United ya Moshono jijini Arusha.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu