Atimae timu ya Azam kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui. Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.






PAMOJA na kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui. Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.



 Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 12 ikiwa na jumla ya michezo sita hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara. Katika mchezo huo bao la Azam FC limefungwa dakika ya tisa na nahodha Himid Mao "Ninja" kwa njia ya mkwaju wa Penalti baada ya beki wa kushoto Bruce Kangwa kuangushwa ndani ya eneo la hatari.



Azam ingeweza kujipatia mabao zaidi ya mawili katika kipindi cha kwanza kama mshambuliaji wake chipukizi, Yahya Zayd na Mbaraka Yusuph wangekuwa makini kutumia nafasi takribani tatu za kufunga mabao.

Comments

Popular posts from this blog

Mtu kadakwa akimpelekea mahabusu simu katika gereza la Keko.

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Hatimae kocha wa timu ya Kagera sugar Meck mexime kumaliza mafunzo ya ukocha amesema akili yake ameiamishia msimu wa ligi kuu Tanzani bara amepanga kuanza mwanzo wa Julai 17mwaka huu