BEKI wa Yanga Andrew Vicent "Dante" amesema kwa sasa safu yao ya ulinzi ipo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na kwamba makosa ya mchezo wa Jumamosi hayatajirudia tena.





BEKI wa Yanga Andrew Vicent "Dante" amesema kwa sasa safu yao ya ulinzi ipo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na kwamba makosa ya mchezo wa Jumamosi hayatajirudia tena. 

Dante amesema wakati huu anaocheza na Kelvin Yonda amejikuta wakifanikiwa kuelewana kwa haraka ambapo hakuna mshambuliaji anayewasumbua. 


Dante alisema Yondani ni moja kati ya mabeki bora na wakongwe ambapo tangu ameanza kucheza naye amejifunza mengi juu ya utulivu wa kuwakabili washambuliaji.


 Alisema mkakati wao wa sasa ni kuhakikisha wanamaliza mechi bila kuruhusu wavu wao kutikiswa, mkakati ambao utaanza katika mchezo dhidi ya Stand Jumapili ijayo.


 “Ligi ni ngumu lakini kwa sasa sisi mabeki tumekuwa na msimamo mkubwa kwamba hatutaki kuona tunaruhusu mabao tunataka kuona kila mchezo tunatoka tukiwa safi hicho ndicho tulichopanga,” alisema Dante

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger