Hatimaye timu ya F stars kuiyaidhibu timu ya KIITEC stars ya jijini Arusha kwa magoli 4-2
Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji Fanikiwa stars imeibuka na ushindi mzito wa mabao manne kwa mawili (4-2) dhidi ya timu ya chuo cha mawasiliano na kompyuta Kiitec united katika uwanja wa chuo hicho uliopo maeneo ya Moshono jijini Arusha. Mchezo huo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza kihistoria siku ya Ijumaa ya tarehe 08 February 2019 , katika dimba hilo la Moshono na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa timu zote mbili huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo. Mchezo ulianza kwa kasi ya aina yake huku Fanikiwa Stars wakiongoza kwa kulishambulia kwa kasi lango la timu ya Kiitek United na baada ya dakika chache tu baada ya mpira kuanza, mchezaji wa Fanikiwa Stars alichezewa rafu katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Patrick Temba akaamuru penati ipigwe na Fanikiwa Stars kuandika bao la kwanza, hadi kipindi cha kwanza kuisha Fanik...