Posts

Hatimaye timu ya F stars kuiyaidhibu timu ya KIITEC stars ya jijini Arusha kwa magoli 4-2

Timu ya chuo cha uandishi wa habari na utangazaji  Fanikiwa stars  imeibuka na ushindi mzito wa mabao manne kwa mawili  (4-2)  dhidi ya timu ya chuo cha mawasiliano na kompyuta  Kiitec united katika uwanja wa chuo hicho uliopo maeneo ya Moshono jijini Arusha. Mchezo huo wa kirafiki uliozikutanisha timu hizo kwa mara ya kwanza kihistoria siku ya Ijumaa ya tarehe  08 February 2019 , katika dimba hilo la Moshono na kuudhuriwa na mamia ya mashabiki wa timu zote mbili huku wengi wao wakiwa ni wanafunzi kutoka katika vyuo hivyo. Mchezo ulianza kwa kasi ya aina yake huku  Fanikiwa Stars  wakiongoza kwa kulishambulia kwa kasi lango la timu ya  Kiitek United  na baada ya dakika chache tu baada ya mpira kuanza, mchezaji wa Fanikiwa Stars alichezewa rafu katika eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo  Patrick Temba akaamuru penati ipigwe na  Fanikiwa Stars  kuandika bao la kwanza, hadi kipindi cha kwanza kuisha Fanik...

Kusaga aacha ujumbe mzito msiba wa Kibonde ‘vijana tuache nyodo, kama uhai ni pesa basi watu wetu wasinge kufa”

Image
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga a metoa ujumbe mzito katika salamu za Clouds Media wakati wa mazishi wa mfanyakazi wao, Kibonde aliyefariki akiwa mkoani Mwanza akipatiwa matibabu. ” Hakuna msanii Mkubwa na maarufu zaidi ya Ruge wala zaidi ya Kibonde kwa hapa Tanzania. Hakika tuache majivuno ulimbukeni wa mali umaarufu na Madaraka Kwani hivi vyote ni vyakupita na tutaviacha Hapa Hapa Duniani. Kama UHAI ungekua ni pesa basi watu wetu wasinge kufa maana tungetafuta pesa kwa namna yeyote ili ili ndg zetu wapone. Lakini hakuna Mtu yeyote Duniani mwenye uwezo wa kununua UHAI wala kuzuwia Mauti. Vijana tupendane sana sana na tuache kujivuna na kujiskia”- Mkurugenzi Mkuu Clouds Media Group’ Joseph Kusaga J Kusaga. RIPkibonde chanzo    BONGO 5

Son Heung-min, aridhia ombi la baba yake, atakiwa kutokuoa mpaka atakapostaafu soka

Image
Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham na timu ya taifa ya Korea Kusini, Son Heung-min amekubali maombi ya baba yake mzazi yanayomtaka asioe mke mpaka pale atakapo staafu soka. Son ambaye anamtazama mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Ronaldo kama role model wake amekuwa na mafanikio mazuri na kuwa chaguo la kwanza la kocha Mauricio Pochettino. Mkorea huyo amesema kuwa baba yake siku zote amekuwa akitamani kumuona akifanikiwa, ilifikia wakati hadi kuadhibiwa yeye na kaka yake kwa kupiga dana dana pale wanapopigana. Staa huyo wa Tottenham amekiambia chombo cha habari cha Guardia, “Hutupatia saa nne za kupiga dana dana sote, ndani ya saa tatu tu naona mipira mitatu mitatu machoni mwangu na ardhi yote nyekundu, nikiwa nimechoka na yeye hukasirika,” amesema Son. Son Heung-min ameongeza “Wakati nilipokuwa na umri wa miaka 10 au 12 na kuja kwa kocha wangu wa timu ya shule na kufanya naye mazoezi tukiwa wachezaji 15 hadi 20. Akiwa na program kwa sisi sote ya kuwa na mpira kwa dakik...

Serikali ya Tanzania yatishia kuufunga mgodi wa Acacia Tarime

Image
Waziri wa Madini Doto Biteko ametishia kuufunga mgodi wa ACACIA North Mara ifikapo Machi 30 mwaka huu, endapo utashindwa kudhibiti maji yenye sumu kwenda kwenye makazi ya watu. Waziri Biteko ameyasema hayo baada kushuhudia kiasi kikubwa cha maji hayo yakielekezwa kwenda maeneo ya wananchi. Tshisekedi na Kabila watangaza serikali ya Muungano R Kelly avunja ukimya Je Mbowe na Matiko wataachiliwa leo? Je, siri za watumiaji wa Facebook zitalindwa kweli? Akizungumza baada ya kukagua miundo mbinu ya maji machafu katika mgodi huo, siku ya Jumanne, waziri huyo ameutaka mgodi huo kuhakikisha tatizo la maji linapatiwa ufumbuzi kabla ya tarehe 30 mwezi Machi. ''Serikali haitajali muwekezaji, sisi maisha ya Mtanzania hata mmoja ni muhimu mno, nyie kwa kuwa mnafanya biashara, mnatakiwa kuzingatia usalama wa watu hapa'' Alisisitiza waziri Biteko. Kwa mujibu wa waziri Biteko, tayari serikali imekwishatuma timu ya wataalamu kukagua mgodi huo, na kwamba wamekwishapewa mu...

Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila waamua kuunda serikali ya muungano

Image
Kiongozi mpya katika Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamesema wameamua kuunda serikali ya muungano kufuatia mazungumzo, shirika la habari la AFP linaripoti. Licha ya ushindi wa rais Tshisekedi -- kiongozi huyo amejikuta akilazimika kugawanya uongozi tangu uchaguzi huo wa urais. Mpaka sasa hajafanikiwa kumteua waziri mkuu kutokana na kwamba muungano wa Kabila - Common Front for Congo (FCC) una uwingi katika bunge la taifa. Je Mbowe na Matiko wataachiliwa leo? Je, siri za watumiaji wa Facebook zitalindwa kweli? R Kelly avunja ukimya Mgomo wa wafanyikazi JKIA ulikuwa na athari gani? Mkwamo huo umeweka kizuizi kwa maazimio ya Tshisekedi kuigeuza nchi hiyo inayogubikwa kwa rushwa na tuhuma za ukiukaji wa haki za binaadamu. Katika taarifa ya pamoja hapo jana Jumatano, Tshisekedi na Kabila wamesema kwamba licha ya "FCC kuwa na uwingi mkubwa bungeni" katika kuidhinisha matakwa yalioelezewa na wapiga kura, FCC na CACH wa...

Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.

Image
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018. Wachezaji watatu waliobaki katika kinyang’anyiro hicho ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni wote wa Simba, ambapo kamati ya Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora imeandaa utaratibu wa kupiga kura kuwashirikisha Wahariri wa Habari za Michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom na makocha wa timu za Ligi Kuu. Pia kamati imekamilisha uteuzi wa wachezaji watakaowania tuzo katika kategori mbalimbali kwenye sherehe hizo za Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL itakayofanyika ukumbi wa Mlimani, City Dares Salaam Juni 23 mwaka huu. Tuzo 16 zinatarajiwa kutolewa siku hiyo, ambapo baadhi ni za kikanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo tayari washindi wake wamefahamika, ambazo ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji bora. Ukiacha hizo tano za kikanuni, zipo tuzo 10 ambazo zimefanyiwa kazi na Kamati ...

Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington.

Image
Shirika la habari la serikali nchini Korea Kaskazini limesema kuwa kiongozi wa taifa hilo Kim Jong Un amekubali mwaliko wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kufika Washington. Kiongozi huyo alipewa mwaliko wakati wa mkutano wa historia baina ya wawili hao nchini Singapore Jumanne. Kim pia alimwalika pia Trump kutembelea Pyongyang. "Viongozi ao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja," shirika la KCNA limeripoti. Kenye tamko lake la kwanza kabisa tangu kutokea kwa mkutano huo, Bw Kim amenukuliwa akisema kwamba kuna haja ya "dharura" ya kusitisha "hatua za kijeshi za uchokozi zinazokera kati ya mataifa" hayo mawili. Alisema nchi zote mbili zinafaa "kujitolea kujizuia kufanya uchokozi" na "kuchukua hatua za kisheria na kitaasisi kuhakikisha hilo linafanyika", KCNA wameripoti. Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribi...