Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018. Wachezaji watatu waliobaki katika kinyang’anyiro hicho ni Emmanuel Okwi, John Bocco na Erasto Nyoni wote wa Simba, ambapo kamati ya Tuzo hiyo ya Mchezaji Bora imeandaa utaratibu wa kupiga kura kuwashirikisha Wahariri wa Habari za Michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom na makocha wa timu za Ligi Kuu. Pia kamati imekamilisha uteuzi wa wachezaji watakaowania tuzo katika kategori mbalimbali kwenye sherehe hizo za Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL itakayofanyika ukumbi wa Mlimani, City Dares Salaam Juni 23 mwaka huu. Tuzo 16 zinatarajiwa kutolewa siku hiyo, ambapo baadhi ni za kikanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo tayari washindi wake wamefahamika, ambazo ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji bora. Ukiacha hizo tano za kikanuni, zipo tuzo 10 ambazo zimefanyiwa kazi na Kamati ...