Posts

Showing posts from August, 2017

UONGOZI wa timu ya Njombe Mji umesema umoja na ushirikiano wa wachezaji katika kikosi hicho utaleta ushindani wa hali ya juu kwa timu watakazocheza nazo Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao.

Image
UONGOZI wa timu ya Njombe Mji umesema umoja na ushirikiano wa wachezaji katika kikosi hicho utaleta ushindani wa hali ya juu kwa timu watakazocheza nazo Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao.  Akizungumza jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Sofanus Mhagama alisema kipindi hiki cha mazoezi wachezaji wameonyesha kuelewana uwanjani na kuyafanyia kazi maelekezo ya walimu kwa kiwango kikubwa.  Alisema ushirikiano wa wachezaji umeongeza chachu kwa kocha wa timu hiyo kuendelea kutoa mbinu mbalimbali za kukifikisha mbali kikosi hicho.  "Wachezaji wanapojituma mwalimu anafarijika na kuona kuwa maelekezo yake yanafutiliwa kwa ukaribu, hicho ndicho kitu tunachojivunia." "Kila mchezaji amepewa majukumu yake na anasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha anayatimiza, hivyo hatuna wasiwasi wowote tupo tayari kwa msimu ujao," alisema Mhagama.

KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.

Image
KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.  Hii ni wiki ya pili sasa Simba imepiga kambi nchini Afrika Kusini ikijifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku lengo kubwa kwa kocha wao huyo raia wa Cameroon likiwa ni kutwaa taji ambalo linashikiliwa na mahasimu wao Yanga. Akizungumza kutoka Johannesburg, kocha Omog alisema mechi hiyo ndiyo iliyompa taswira kamili ya ubora wa kikosi chake baada ya kufanya mazoezi magumu kwa muda wote ambao wapo nchini humo.  “Nimependekeza kucheza na timu hii kwa sababu ndiyo kipimo kizuri kwa mazeozi ambayo tumeyafanya hapa nchini lakini kitu kikubwa kwangu sio kuangalia matokeo bali ninachotaka kuona ni namna gani wachezaji wameyashika yale tuliyoyafundisha na jinsi wanavyoyafanyia kazi,” alisema Omog. Omog alisema kwa maandalizi waliyoy...

ATHUMANI Idd "Chuji" amerejea Ligi Kuu bara baada ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara. Chuji amerejea kwa kusaini mkataba wa mweaka mmoja kuichezea Ndanda ambayo msimu uloipita ilifanya kazi ya ziada kubaki Ligi Kuu Bara. Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alipotea baada ya kuachwa na Yanga misimu mitano iliyopita.

Image
ATHUMANI Idd "Chuji" amerejea Ligi Kuu bara baada ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara. Chuji amerejea kwa kusaini mkataba wa mweaka mmoja kuichezea Ndanda ambayo msimu uloipita ilifanya kazi ya ziada kubaki Ligi Kuu Bara. Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alipotea baada ya kuachwa na Yanga misimu mitano iliyopita.  Juhudi zake za kutaka kurejea Ligi Kuu Bara zilionyesha kutokuwa na mafanikio hata alipojiunga na Mwadui FC ya Shinyanga ambayo licha ya kukaa misimu miwili, hakupata nafasi ya kucheza. Baada ya hapo Chuji aliamua kijiweka kando mwa Ligi hiyo na hivi karibuni alii buka na kufanya vizuri katika michuano ya Ndondo FC.

Hatimae kocha wa Panone FC jumanne Ntambi amejiunga na mwadui fc kuchukua nafasi ya Ali Bushir

Image
ALIYEKUWA kocha wa Panone FC, Jumanne Ntambi amejiunga na Mwadui FC kuchukua nafasi ya Ali Bushir aliyetupiwa virago.  Ntambi aliyewahi kuifundisha Mwadui miaka ya nyuma, amesaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao. Katibu mkuu wa Mwadui, Ramadhani Kilao alisema Kocha huyo ataungana na Khalid Adam aliyekuwa kocha msaidizi wa Julio na Bushir.  Alisema kuwa kati ya makocha hao, baada ya kusaini mkataba wanaangalia nani atakuwa kocha mkuu kwa sababu wote wanalingana kiwango cha elimu ambacho ni leseni ‘B’. “Baada ya kumuondoa Bushir tumemleta kocha mwingine anaitwa Ntambi, anaendelea na mazoezi na timu lakini kesho (juzi), ndio atasaini mkataba ila tutaangalia nani atakuwa kocha mkuu yeye na Khalid,” alisema Kilao.

Hatimae simba wiki hii simba yapokea kichapo na timu ya wenyeji wao wa afrika kusini katika kujipima nguvu

Image
VIGOGHO wa Soka Tanzania, Simba SC mapema wiki hii wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu katika kambi yao ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Orlando Pietes.  Kwa mujibu wa msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon Joseph Omog ilicheza vizuri pamoja na kufungwa.  “Kwa mujibu wa maelezo ya benchi la ufundi mchezo ulikuwa mzuri na timu ilicheza vizuri lakini bahati ilikuwa kwa wenyeji wao kupata ushindi huo," amesema Manara. Manara amesema Omog anayesaidiwa na Mganda Jackson Mayanja aliwapa nafasi karibu wachezaji wote kucheza akipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi.

WACHEZAJI wa zamani wa Yanga, Omega Seme na mlinzi Busungu wamejihakikishia maisha ndani ya kikosi cha Lipuli FC baada ya kusaini mkataba wa miaka mmoja kwa kila mmoja. Busungu aliyemaliza na Yanga msimu uliopita hakuweza kuongezewa mkataba baada ya kushindwana na uongozi na hivyo kuwa mchezaji huru.

Image
WACHEZAJI wa zamani wa Yanga, Omega Seme na mlinzi Busungu wamejihakikishia maisha ndani ya kikosi cha Lipuli FC baada ya kusaini mkataba wa miaka mmoja kwa kila mmoja. Busungu aliyemaliza na Yanga msimu uliopita hakuweza kuongezewa mkataba baada ya kushindwana na uongozi na hivyo kuwa mchezaji huru.  Kocha mkuu Lipuli FC, Seleman Matola alisema tayari wachezaji wamesajiliwa na timu hiyo na kuungana na wenzao katika kambi yao iliyopo Iringa. “Tunashukuru mazungumzo yamekwenda vizuri, Busungu pamoja na Omega ni wachezaji wetu halali na wameungana na wenzao Alhamisi kwenye mazoezi ya kujiwinda na Ligi Kuu, ” alisema Matola. Aliongeza kikosi chake kitakua na wachezaji mchanganyiko wakiwemo wakongwe ambao watasaidia kuimalisha timu hiyo ili iweze kukabiliana na mikiki ya ushindani kwa timu kubwa. Matola aliongeza baada ya wiki moja wanatarajia kuwa na mechi za kirafiki dhidi ya Mbeya City, Njombe Mji pamoja na Singida United.