MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini. Kila timu imeshaangusha pointi Ni timu tano tu ambazo hazijapoteza mchezo katika ligi kuu msimu huu. Mtibwa, Azam FC, Simba, mabingwa watetezi Yanga na Tanzania Prisons, lakini zote hizo tayari zimeangusha pointi msimu huu huku Mtibwa na Azam FC wakiwa pekee waliangusha alama chache (mbili) baada ya kila timu kucheza michezo minne. Simba tayari wameangusha pointi nne, sawa na Yanga na Prisons ambazo zimeshinda michezo miwili na kupata sare katika michezo mingine miwili. Hii inamaanisha ligi imeanza kwa ugumu licha ya washambuliaji kuonekana kuwa na ‘usongo’ wa kufumania nyavu. Wakati Mtibwa wakiangusha alama mbili Jumapili iliyopita mbe...