Posts

ATIMAE MOHAMED SALAH AVUNJA REKODI YA LIVERPOOL

Image
Jana majogoo wa London klabu ya Liverpool walithibitisha kumsajili winga wa As Roma Mohed Salah ambaye walimtafuta kwa muda sasa kwa dau la euro million 39. Hii sio mara ya kwanza kwa Salah kucheza katika ligi kuu nchini Uingereza kwani hapo mwanzo kabla hajahamia nchini Italia aliwahi kukipiga na timu ya Chelsea. Mohamed Salah amesema ujio wake Liverpool ni tofauti na Chelsea kwani kipindi wakati anaenda Chelsea alikuwa bado mtotomtoto lakini sasa anajiona ni bora zaidi. “Nina uhakika 100% kwamba kila kitu kimebadilika hadi muonekano wangu,kipindi kile nilikuwa na miaka 20 ila sasa nina 24 na nina uzoefu mkubwa zaidi tofauti na hapo mwanzo” alisema Salah. Mkataba wa Salah na Liverpool utamfanyia kila mwisho wa wiki kuweka kiasi cha euro 90,000 huku akikabidhiwa jezi namba 11 na Firminho akipewa jezi namba 9. Usajili wa Mohamed Salah wa euro million 39  umevunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Andy Caroll aliyesajiliwa kwa euro milion 35 ...

gari la ajabu

Image

Wanyama na siri ya jezi namba 67 mgongoni

Image
Wachezaji wengi wa hususan soka ukiwauliza kwanini anavaa jezi yenye namba fulani mgongoni atakupa history nyuma ya namba hiyo, wengi wao hawavai kama urembo au ilimradi tu ni namba. wapo wengine kabla ya kusajiliwa na timu wanazozihitaji hutoa masharti kwamba akifika klabuni ni lazima apewe jezi yenye namba anayoitaka, mfano mzuri ni Michael Ballack wakati anasajiliwa Chelsea alitaka namba 13 ambayo wakati huo ilikuwa inavaliwa na Gallas ambaye alikataa kubadilisha jezi matokeo yake ikalazimika kuondoka kumpisha Ballack aje avae jezi namba 13. kwa upande wa mkenya Victor Wanyama, yeye alivyosajiliwa Celtic ya Scotland alichagua kuvaa jezi namba 67 ambayo ni namba kubwa, lakini alifanya hivyo makusudi kabisa na haikuwa bahati mbaya. Kupitia Sports Extra ya Clouds FM, Wanya,ma ametaja sababu kubwa iliyomfanya aache namba nyingine zote na kuchagua namba 67 ambayo kiuhalisia ipo mbali sana. “Kila mchezaji ana ndoto, kwa hiyo nilivyokwenda pale nikikuwa na ndoto na nilikuwa naju...

Trump akana kumrekodi aliyekuwa mkurugenzi wa FBI

Image
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa hakumrekodi aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la FBI James Comey licha ya kudai hivyo hapo awali. Alituma ujumbe katika mtandao wake wa Twitter kwamba hakutengeza na wala hana rekodi hizo siku moja baada ya kutakiwa kuwasilisha kanda hizo kwa jopo la Congress. Bwana Trump alianzisha uvumi wa rekodi hizo katika ujumbe wa Twitter aliochapisha siku moja baada ya kumfuta kazi bwana Comey mnamo mwezi Mei. Alisema: James Comey uwe na matumaini kwamba sina sina rekodi zozote za sauti yako kuhusu mazungumzo yetu. Chapisho hilo lilizua madai chungu nzima kwamba bwana Comey alifutwa kazi ili kuzuia uchunguzi kuhusu Urusi kuingilia Uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita mbali na ushirikiano wake na kampeni ya rais Donald Trump mjini Moscow. Licha ya lengo lake kutobainika, ujumbe huo wa Twitter ulisababisha kuajiriwa kwa mtaalam ambaye amechukua uongozi wa uchunguzi wa madai hayo. Swala hilo linatokana na uchaguzi wa urais wa mwaka jana na...

Korea Kaskazini yafanyia majaribio mashine zake

Image
Maafisa wa Marekani wanaamini kwamba Korea kaskazini ilitekeleza jaribio jingine la mashine ya kurushia makombora yake . Jaribio hilo linadaiwa kutekelezwa siku ya Jumatano litakuwa jaribio la kwanza la mashine kama hiyo kutekelezwa na Korea Kaskazini tangu mwezi Machi. Habari hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi kati ya washington na Pyongyang kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea kaskazini. Utawala wa Trump umefanya swala hilo kuwa swala kuu. Korea Kaskazini yarusha makombora tena Korea Kaskazini: Tulifanyia majaribio makombora mapya Korea Kaskazini: Tutafanya majaribio kila wiki Licha ya shutuma za kimataifa ,Korea Kaskazini imeongeza majaribio yake ya makombora kwa lengo la kutengeza kombora linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine. Shirika la ujasusi la Marekani limeonya mwezi uliopita kwamba Korea Kaskazini linakaribia kufanikiwa katika mpango huo. Maafisa wa Marekani waliokuwa wakizungumza kwa vitengo kadhaa vya habari walisema hatua hiyo ya hivi k...

Madiwani na Naibu Meya CHADEMA Watiwa Mbaroni Arusha

Image
Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viola Likindikoki, pamoja na madiwani wengine wawili wa Chadema wamekamatwa jana na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa sababu ambazo mpaka sasa hazijafahamika. Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro amesema Viola pamoja na madiwani hao wawili walikamatwa  jana Alhamisi  wakiwa katika mkutano wa ndani uliokuwa ukisikiliza kero za wananchi. “Nipo Tanga kikazi na nilimkaimisha nafasi yangu Viola, kwa kawaida Alhamisi tunasikiliza kero za wananchi, wakati wakiendelea kusikiliza kero ndipo walipokamatwa,” alisema. Wengine waliokamatwa katika tukio hilo ni diwani wa viti maalumu (Chadema), Kata ya Ngarenaro Happiness Charles na diwani wa Viti Maalumu kata ya Olorieni, Sabrina Francis. Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Charles Mkumbo amesema kwa kifupi kwamba jeshi lake linawashikilia kwa uchunguzi. Diwani wa viti maalumu (Chadema), Jenipher Lomayan  amesema madiwani hao walikamatwa   jana saa 9 alasiri  wakiwa ndani...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 23

Image