Posts

Mgomo wasababisha ghasia kali Venezuela

Image
Mamilioni ya Wavenezuela wameitikia wito wa Upinzani wa kubakia nyumbani, katika mgomo wa kwanza wa saa 24 kufanyika nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja. Hatua hiyo ni kupinga mipango ya serikali ya kuandika tena katiba mpya. Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi katika miji kadhaa, walipopambana na waandamanaji. Katika ghasia hizo waandamanaji watatu waliuawa. Hata hivyo, katika maeneo yanayounga mkono serikali ya nchi hiyo mjini Caracas, maisha yaliendelea kama kawaida. Katika hotuba yake kupitia televisheni, Rais Nicolas Maduro amesema mamia ya wafanyabiashara waliendelea na shughuli zao kama kawaida na kwamba viongozi wa mgomo huo watakamatwa. Lakini upinzani nao umedai kuwa Rais Maduro anajaribu kujiimarisha madarakani kwa kubadili katiba, hali ambayo itabadili hali ya sasa ya upinzani kudhibiti bunge. Na katika Umoja wa Mataifa mwanadiplomasia wa Venezuela amejiuzulu katika kupinga hatua zinazochukuliwa na serikali yake.
Image
Vijana sita wa Burundi waliokuwa wakishiriki katika mashindano ya roboti nchini Marekani wameripotiwa kutoweka, polisi wanasema. Wavulana wanne na wasichana 2 walio kati ya umri wa miaka 16 na 18 walipotea wakati wa mashindano hayo ya kwanza duniani yaliofanyika Washington DC. Idara ya polisi mjini humo imesema kuwa mara ya mwisho vijana hao kuonekana ilikuwa siku ya Jumanne wakati wa makamilisho ya michezo hiyo. Ripoti zinasema kuwa vijana wawili kati yao tayari wamevuka mpaka na kuingia Canada lakini ripoti hiyo haijathibitishwa na polisi. Nkurunziza afika Tanzania ziara yake ya kwanza nje tangu 2015 Nkurunziza aashiria kuwania muhula wa nne Burundi Wafungwa wengi waachiliwa Burundi Siku ya Alhamisi, idara ya polisi mjini humo ilibandika picha za sura za vijana hao sita waliopotea katika mtandao wao wa Twitter, wakiwataka raia kuwasiliana nao iwapo watakuwa na habari yoyote kuwahusu. Vijana hao wanatambulika kuwa Don Ingabire, Kevin Sambukiza, Nice Munezero, Audry M...

Caf yasikia kilio cha Mourinho na Klopp

Image
Kwa muda mrefu makocha wa ligi kubwa barani Ulaya wamekuwa wakulalamikia utaratibu wa chama cha soka Afrika CAf kufanya mashindano ya mataifa ya Afrika Afcon wakati ligi zikiwa zinaendelea. Hii imekuwa ikizigharimu sana klabu za barani Ulaya kwa kuwakosa wachezaji wao muhimu wa Kiafrika wakati ligi ikiwa inaendelea lakini sasa shirikisho la mpira wa miguu Afrika Caf limesikia kilio cha vilabu hivyo. Caf wameamua kuanzia sasa michuano hiyo mikubwa Afrika itakuwa ikifanyika mwezi June hadi July tofauti na mwanzo ambapo michuano hiyo ilikuwa ikifanyika kuanzia mwezi January hadi February. Kuanzia mwaka 2019 ambapo mashindano hayo yatachezwa nchini Cameroon ratiba itabadilika huku timu zitakzoshiriki michuano hiyo nazo  zikiongezeka kutoka timu 16 kama ilivyokuwa mwanzo hadi timu 24. Makocha wa vilabu vya Uingereza akiwemo Jose Mourinho na Jurgen Klopp walikuwa wahanga wakubwa wa michuano ya Afcon lakini sasa watakuwa wamesaidiwa kwa kiasi kikubwa kubaki na wachezaji wao. ...

yaliyo jiri magazetini

Image

Hatimae m bunge wa Temeke kupandishwa kizimbani na kulipa faini ya pound 100 na tsh 30,000

Image
Mbunge wa Temeke Mhe. Abdalah Mtolea jana alipandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Temeke akikabiliwa na mashataka mawili ikiwemo la kuendesha gari bila ya bima kinyume na sheria za nchi. Mbunge huyo kwa tiketi ya chama cha wanachi CUF, alisomewa mashtaka yake mbele ya hakimu mkazi Mhe. Eliarusia Nassatri mbale ya mwendesha mashtaka wa serikali Joseph Maugo ambaye aliiambia mahakama hiyo kuwa katika kosa la kwanza Mbunge huyo anadaiwa kuendesha gari ambalo halina bima Maelezo ya kosa hilo yanadai kuwa, Julai 19 mwaka huu katika barabara ya Kilwa eneo la Bendera tatu, mshtakiwa alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 672 BNV Toyota Mark 2 likiwa halina bima. Katika kosa la pili, mshatakiwa Mtolea anadaiwa kulitenda muda na eneo la kwanza alipotenda kosa la kwanza kwakushindwa kutekeleza agizo la ofisa Polisi mwenye namba F 818 Kopla Robati la kutakiwa kupeleka gari hilo katika kituo cha Polisi Kilwa Road lakini mshtakiwa alikaidi agizo hilo na kuelekea...
Image
KATIBU mkuu wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, Yanga, Charles Boniface Mkwasa ametoa pole kwa wanachama wa klabu ya Simba kufuatia matatizo yaliyowakumba na kusababisha baadhi ya viongozi wake wa ngazi za juu kufikishwa kwenye vyombo vya dola.  Baadhi ya viongozi wa juu wa klabu ya Simba ambao wapo mahabusu ni pamoja na rais wake, Evas Aveva na makamu mwenyekiti Geoffrey Nyange “Kaburu”.  “Sisi wote ni familia ya soka hatuwezi kufurahia matatizo yanayowapata viongozi wa Simba wakati huu, suala hili limetugusa na tunawapa pole wanachama wao.”  “Hatuna uadui nje ya uwanja, vita yetu ni ya kimpira tu, hivyo yanapotokea matatizo kama haya tunakuwa bega kwa bega katika kufarijiana na kutiana moyo,” alisema Mkwasa. Kesi ya viongozi hao imepangwa kusomwa tena Julai 20, mwaka huu kwenye mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Image
KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Ramadhan Singano (Messi) amemuwahi mwenzake Simon Msuva baada ya kuondoka nchini juzi kujiunga na klabu ya Difaa Hassan D’Eljadida iliyoshiriki ligi kuu nchini Morocco.  Messi ambaye mkataba wake umemalizika hivi karibuni na klabu yake ya Azam amekwenda nchini Morocco kwa ajili ya kujiunga na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo yenye timu 16.  Wakati Messi akiondoka nchini humo winga wa Yanga, Simon Msuva ambaye naye anapigiwa hesabu na klabu hiyo anatarajia kuondoka nchini alhamisi hii ili kujiunga na klabu hiyo.  Meneja wa Azam, Philp Alando alipoulizwa kuhusu safari ya winga huyo alisema kuwa klabu hiyo aina taarifa na lolote lile kwa kuwa walimalizana naye toka mkataba wake umemalizika.  “Mkataba wa Singano ulikuwa umemalizika Julai 8 mwaka huu hivyo sisi hatuna mazungumzo naye yoyote na wala hatujui kuhusu safari hiyo ya Morocco wala chochote kinachoendelea,” alisema.  Wakati ...