Posts

Showing posts from 2017

Atimae timu ya Azam kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui. Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.

Image
PAMOJA na kwenda kwa kujiamini katika mchezo wa ugenini, timu ya Azam FC imejikuta ikivutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na timu ya Mwadui. Mechi hiyo ilichezwa juzi katika uwanja wa Mwadui Complex na kuishuhudia Azam FC ikiendelea kugandwa na jinamizi la sare.  Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha jumla ya pointi 12 ikiwa na jumla ya michezo sita hadi sasa kwenye Ligi Kuu Bara. Katika mchezo huo bao la Azam FC limefungwa dakika ya tisa na nahodha Himid Mao "Ninja" kwa njia ya mkwaju wa Penalti baada ya beki wa kushoto Bruce Kangwa kuangushwa ndani ya eneo la hatari. Azam ingeweza kujipatia mabao zaidi ya mawili katika kipindi cha kwanza kama mshambuliaji wake chipukizi, Yahya Zayd na Mbaraka Yusuph wangekuwa makini kutumia nafasi takribani tatu za kufunga mabao.

BEKI wa Yanga Andrew Vicent "Dante" amesema kwa sasa safu yao ya ulinzi ipo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na kwamba makosa ya mchezo wa Jumamosi hayatajirudia tena.

Image
BEKI wa Yanga Andrew Vicent "Dante" amesema kwa sasa safu yao ya ulinzi ipo katika mkakati mkubwa wa kuhakikisha nyavu zao hazitikiswi na kwamba makosa ya mchezo wa Jumamosi hayatajirudia tena.  Dante amesema wakati huu anaocheza na Kelvin Yonda amejikuta wakifanikiwa kuelewana kwa haraka ambapo hakuna mshambuliaji anayewasumbua.  Dante alisema Yondani ni moja kati ya mabeki bora na wakongwe ambapo tangu ameanza kucheza naye amejifunza mengi juu ya utulivu wa kuwakabili washambuliaji.  Alisema mkakati wao wa sasa ni kuhakikisha wanamaliza mechi bila kuruhusu wavu wao kutikiswa, mkakati ambao utaanza katika mchezo dhidi ya Stand Jumapili ijayo.  “Ligi ni ngumu lakini kwa sasa sisi mabeki tumekuwa na msimamo mkubwa kwamba hatutaki kuona tunaruhusu mabao tunataka kuona kila mchezo tunatoka tukiwa safi hicho ndicho tulichopanga,” alisema Dante

Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu.

Image
Wapiga kura waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura watapata fursa ya kupiga kura katika uchaguzi mdogo wa madiwani wa kata 43 unaotarajiwa kufanyika Novemba 26, mwaka huu. Hayo yamesemwa jana Jumatatu Oktoba 16, 2017 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima mjini Dodoma ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi yanayoratibiwa na kuendeshwa na NEC. Kailima alisema wapiga kura hao wataruhusiwa kutumia vitambulisho vya uraia vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), hati ya kusafiria na leseni ya udereva. “Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia kifungu namba 62 (a) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambacho kinasema mpiga kura aliyeandikishwa kwenye daftari atakwenda mwenyewe kwenye kata aliyojiandikisha, kwenye kituo alichopangiwa, kumridhisha msimamizi wa kituo au msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwamba yeye ndiye mpiga kura kwa kumuonyesha kadi ...

VIWANJA VINA UZWA KWA BEI NAFUU

Image
Kiwanja kinaunzwa  na vimepimwa  na serekali  na kipo barabarani  na kuna njia ya mitaa   Bara bara ya kwenda hadi kwenye kiwanja chako  mteja inapita hadi gari ukubwa wa kiwanja kw mawasiliano 0712597387

MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini.

Image
MTIBWA Sugar FC iliangusha pointi za kwanza baada ya kucheza mchezo wa nne msimu huu. Baada ya kuzishinda timu tatu kutoka Kanda ya Ziwa (Stand United, Mwadui FC, Mbao FC) mabingwa hao mara mbili wa zamani walilazimika kusawazisha goli la Zubery Daby na kupata sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting ya Pwani katika mchezo wao wa kwanza ugenini. Kila timu imeshaangusha pointi Ni timu tano tu ambazo hazijapoteza mchezo katika ligi kuu msimu huu. Mtibwa, Azam FC, Simba, mabingwa watetezi Yanga na Tanzania Prisons, lakini zote hizo tayari zimeangusha pointi msimu huu huku Mtibwa na Azam FC wakiwa pekee waliangusha alama chache (mbili) baada ya kila timu kucheza michezo minne. Simba tayari wameangusha pointi nne, sawa na Yanga na Prisons ambazo zimeshinda michezo miwili na kupata sare katika michezo mingine miwili. Hii inamaanisha ligi imeanza kwa ugumu licha ya washambuliaji kuonekana kuwa na ‘usongo’ wa kufumania nyavu. Wakati Mtibwa wakiangusha alama mbili Jumapili iliyopita mbe...

Atimae timu ya mtibwa sugar inaongoza lingi ikiwa na pointi 10

Image
Timu ya Mtibwa Sugar inaongoza ligi ikiwa na pointi 10, lakini baadhi ya mashabiki na wadau wa soka wamekuwa wakiibeza timu hiyo kuwa wamewashikia nafasi baadhi ya vilabu. saria news imemtafuta kocha mkuu wa timu hiyo Zuber Katwila ambaye amesema, wanaoibeza timu yake kuwa wameshika nafasi za watu wasubiri wataona kitakachotokea. “Mimi mwenyewe nimekuwa nikizisikia hizo taarifa watu wakitubeza lakini wanatakiwa watambue kuwa hii ligi haina mwenyewe, kila timu inaweza kuwa bingwa kwa hiyo kama wataendelea kutubeza bila kufanya vizuri wataona kitakachotokea,” Katwila. Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa Jumamosi Uhuru, amesema anafanya maandalizi na kikosi chake kama mechi zingine za ligi huku akiongeza mbinu za kumfanya atoke na ushindi. “Ni mechi ngumu ambayo inaweza kutupandisha ama kutushusha kutokana na pointi zetu zilivyo, lakini mimi na wenzangu tunakiandaa kikosi vizuri kama mechi zingine, tumerudi Manungu kwa ajili ya maandalizi zaidi na ndio ...

Ilipo fika tarehe Tarehe 18 October mwaka 2000 Bayern Munich walikutana na PSG ambapo Bayern Munich waliichapa PSG mabao 2 kwa 0, leo miaka 7 baadae vigogo hawa wanakutana katila dimba la Pac Des Princes nchini Ufaransa.

Image
Tarehe 18 October mwaka 2000 Bayern Munich walikutana na PSG ambapo Bayern Munich waliichapa PSG mabao 2 kwa 0, leo miaka 7 baadae vigogo hawa wanakutana katila dimba la Pac Des Princes nchini Ufaransa. PSG wanaikaribisha Bayern Munich huku wakipewa nafasi kubwa kuibuka kidedea kutokana na kuwa fowadi kiwembe inayoongozwa na Edison Cavvani, Neymar na Kylian Mbappe. Bayern Munich wana rekodi nzuri kubeba Champions League kuliko PSG na hii leo watategemea kumuona Roberto Lewandoski akiwabeba, huku mshambuliaji huyo msimu huu akifunga jumla ya mabao 11 katika mashindano yote. Psg wamekuwa na rekodi nzuri katika uwanja wao wa Pac Des Princes ambapo katika michezo 43 ya Ulaya waliyocheza katika dimba hilo wamepoteza mchezo mmoja tu na leo pia watamkaribisha winga Kingsley Koman ambaye alianza maisha yake ya soka akiwa na PSG. Group D moto unawaka kwani Juventus hawana point hata moja na leo watatafuta pointi dhidi ya vibonde wenzao wa kundi Olympiacos, huku vinara wa kundi D B...

chirwa akabidhiwa mchezaji Amissi Tambwe ambaye sasa ni majeruhi alisema kocha mkuu wa yanga George Lwandamila

Image
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amemkabidhi Obrey Chirwa majukumu ya Amissi Tambwe ambaye kwa sasa ni majeruhi. Chirwa amepewa majukumu hayo kutokana na Tambwe kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti. Kutokana na kuuguza majeraha hayo, ilisababisha Tambwe akose mechi tano za kimashindano ambazo tayari Yanga imecheza ikiwa moja ya Ngao ya Jamii na nne Ligi Kuu Bara. “Kukosekana kwa Tambwe hakuna tatizo lolote lile kwani Chirwa yupo, ninachokifanya ni kwamba kwenye kikosi changu natengeneza ile hali kwamba akikosekana mmoja basi anakuwepo mwingine wa kuziba pengo lake,” alisema Lwandamina.

UONGOZI wa timu ya Njombe Mji umesema umoja na ushirikiano wa wachezaji katika kikosi hicho utaleta ushindani wa hali ya juu kwa timu watakazocheza nazo Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao.

Image
UONGOZI wa timu ya Njombe Mji umesema umoja na ushirikiano wa wachezaji katika kikosi hicho utaleta ushindani wa hali ya juu kwa timu watakazocheza nazo Ligi Kuu Tanzania bara msimu ujao.  Akizungumza jana, Ofisa Habari wa timu hiyo, Sofanus Mhagama alisema kipindi hiki cha mazoezi wachezaji wameonyesha kuelewana uwanjani na kuyafanyia kazi maelekezo ya walimu kwa kiwango kikubwa.  Alisema ushirikiano wa wachezaji umeongeza chachu kwa kocha wa timu hiyo kuendelea kutoa mbinu mbalimbali za kukifikisha mbali kikosi hicho.  "Wachezaji wanapojituma mwalimu anafarijika na kuona kuwa maelekezo yake yanafutiliwa kwa ukaribu, hicho ndicho kitu tunachojivunia." "Kila mchezaji amepewa majukumu yake na anasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha anayatimiza, hivyo hatuna wasiwasi wowote tupo tayari kwa msimu ujao," alisema Mhagama.

KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.

Image
KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema baada ya timu yake kucheza mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatano hii na kufungwa bao 1-0, ameanza kuona mwanga wa kupata kikosi kipya cha kwanza cha wachezaji 11.  Hii ni wiki ya pili sasa Simba imepiga kambi nchini Afrika Kusini ikijifua kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku lengo kubwa kwa kocha wao huyo raia wa Cameroon likiwa ni kutwaa taji ambalo linashikiliwa na mahasimu wao Yanga. Akizungumza kutoka Johannesburg, kocha Omog alisema mechi hiyo ndiyo iliyompa taswira kamili ya ubora wa kikosi chake baada ya kufanya mazoezi magumu kwa muda wote ambao wapo nchini humo.  “Nimependekeza kucheza na timu hii kwa sababu ndiyo kipimo kizuri kwa mazeozi ambayo tumeyafanya hapa nchini lakini kitu kikubwa kwangu sio kuangalia matokeo bali ninachotaka kuona ni namna gani wachezaji wameyashika yale tuliyoyafundisha na jinsi wanavyoyafanyia kazi,” alisema Omog. Omog alisema kwa maandalizi waliyoy...

ATHUMANI Idd "Chuji" amerejea Ligi Kuu bara baada ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara. Chuji amerejea kwa kusaini mkataba wa mweaka mmoja kuichezea Ndanda ambayo msimu uloipita ilifanya kazi ya ziada kubaki Ligi Kuu Bara. Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alipotea baada ya kuachwa na Yanga misimu mitano iliyopita.

Image
ATHUMANI Idd "Chuji" amerejea Ligi Kuu bara baada ya kujiunga na Ndanda FC ya Mtwara. Chuji amerejea kwa kusaini mkataba wa mweaka mmoja kuichezea Ndanda ambayo msimu uloipita ilifanya kazi ya ziada kubaki Ligi Kuu Bara. Kiungo huyo wa zamani wa Yanga alipotea baada ya kuachwa na Yanga misimu mitano iliyopita.  Juhudi zake za kutaka kurejea Ligi Kuu Bara zilionyesha kutokuwa na mafanikio hata alipojiunga na Mwadui FC ya Shinyanga ambayo licha ya kukaa misimu miwili, hakupata nafasi ya kucheza. Baada ya hapo Chuji aliamua kijiweka kando mwa Ligi hiyo na hivi karibuni alii buka na kufanya vizuri katika michuano ya Ndondo FC.

Hatimae kocha wa Panone FC jumanne Ntambi amejiunga na mwadui fc kuchukua nafasi ya Ali Bushir

Image
ALIYEKUWA kocha wa Panone FC, Jumanne Ntambi amejiunga na Mwadui FC kuchukua nafasi ya Ali Bushir aliyetupiwa virago.  Ntambi aliyewahi kuifundisha Mwadui miaka ya nyuma, amesaini mkataba wa kukinoa kikosi hicho kwa msimu ujao. Katibu mkuu wa Mwadui, Ramadhani Kilao alisema Kocha huyo ataungana na Khalid Adam aliyekuwa kocha msaidizi wa Julio na Bushir.  Alisema kuwa kati ya makocha hao, baada ya kusaini mkataba wanaangalia nani atakuwa kocha mkuu kwa sababu wote wanalingana kiwango cha elimu ambacho ni leseni ‘B’. “Baada ya kumuondoa Bushir tumemleta kocha mwingine anaitwa Ntambi, anaendelea na mazoezi na timu lakini kesho (juzi), ndio atasaini mkataba ila tutaangalia nani atakuwa kocha mkuu yeye na Khalid,” alisema Kilao.

Hatimae simba wiki hii simba yapokea kichapo na timu ya wenyeji wao wa afrika kusini katika kujipima nguvu

Image
VIGOGHO wa Soka Tanzania, Simba SC mapema wiki hii wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza wa kujipima nguvu katika kambi yao ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya baada ya kufungwa 1-0 na wenyeji, Orlando Pietes.  Kwa mujibu wa msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara Simba inayofundishwa na kocha Mcameroon Joseph Omog ilicheza vizuri pamoja na kufungwa.  “Kwa mujibu wa maelezo ya benchi la ufundi mchezo ulikuwa mzuri na timu ilicheza vizuri lakini bahati ilikuwa kwa wenyeji wao kupata ushindi huo," amesema Manara. Manara amesema Omog anayesaidiwa na Mganda Jackson Mayanja aliwapa nafasi karibu wachezaji wote kucheza akipanga vikosi viwili tofauti kila kipindi.

WACHEZAJI wa zamani wa Yanga, Omega Seme na mlinzi Busungu wamejihakikishia maisha ndani ya kikosi cha Lipuli FC baada ya kusaini mkataba wa miaka mmoja kwa kila mmoja. Busungu aliyemaliza na Yanga msimu uliopita hakuweza kuongezewa mkataba baada ya kushindwana na uongozi na hivyo kuwa mchezaji huru.

Image
WACHEZAJI wa zamani wa Yanga, Omega Seme na mlinzi Busungu wamejihakikishia maisha ndani ya kikosi cha Lipuli FC baada ya kusaini mkataba wa miaka mmoja kwa kila mmoja. Busungu aliyemaliza na Yanga msimu uliopita hakuweza kuongezewa mkataba baada ya kushindwana na uongozi na hivyo kuwa mchezaji huru.  Kocha mkuu Lipuli FC, Seleman Matola alisema tayari wachezaji wamesajiliwa na timu hiyo na kuungana na wenzao katika kambi yao iliyopo Iringa. “Tunashukuru mazungumzo yamekwenda vizuri, Busungu pamoja na Omega ni wachezaji wetu halali na wameungana na wenzao Alhamisi kwenye mazoezi ya kujiwinda na Ligi Kuu, ” alisema Matola. Aliongeza kikosi chake kitakua na wachezaji mchanganyiko wakiwemo wakongwe ambao watasaidia kuimalisha timu hiyo ili iweze kukabiliana na mikiki ya ushindani kwa timu kubwa. Matola aliongeza baada ya wiki moja wanatarajia kuwa na mechi za kirafiki dhidi ya Mbeya City, Njombe Mji pamoja na Singida United.

Yaliyo jili magazetini hii leo tarehe 25/7/2017

Image

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake.

Image
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake. Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri. Mawakili watano wa upande wa Jamhuri waloshiriki katika kesi hiyo, waliiambia Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la jinai Julai 17 mwaka huu katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Lissu ambaye alikuwa akitetewa na jopo la mawakili 20 wakiongozwa na Fatma Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge huyo pia alisikika akisema, “kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.” Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 27 ambapo hatma ya dhamana ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) itakapojulikana.

Shirika la TRA imeipelekea madai yake katika kampuni yam Acacia imeiambia kuwa wanadaiwa kodi ya kwanzia mwaka 2000 hadi 2017 hadi 2017 na pangea inadaiwa kodi ya kati ya mwaka 2007 hadi 2017 yenye dhamani ya shilingiTrilioni 425 .......

Image
Kampuni ya Acacia imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inayoonyesha kuwa migodi yake ya Bulyanhulu inadaiwa kodi ya kati ya mwaka 2000 hadi 2017 na Pangea inadaiwa kodi ya kati ya 2007-2017. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Acacia jana Julai 24, imeeleza kuwa taarifa hiyo imetokana na ripoti za kamati mbili za Rais zilizoonyesha kuwa wamekuwa hawatangazi kiasi halisi cha mapato yao wakisafirisha mchanga kwenda nje ya nchi. Acacia wamesema kuwa, bado wanaendelea na msimamo wao wa kupinga matokeo ya kamati hizo na kusema kuwa wamekuwa wakitangaza mapato yao.  Aidha, wameeleza kwamba bado hawajapata nakala za ripoti za kamati ya kwanza na ya pili zilizowasilishwa kwa Rais Magufuli Mei 24 na Juni 12 mwaka huu. Uchambuzi uliofanywa na TRA umeonyesha kuwa Mgodi wa Bulyanhulu unadaiwa na serikali takribani Tsh 344.8 trilioni (USD 154bn) na Mgodi wa Pangea takribani Tsh 76.1 trilioni (USD 36bn). Uchambuzi huo una...

Hatimae real Madrid ya fungwa na Manchester united kwa mikwaju ya penati na kumaliza dakika 90 sare ya magoli 1-1...........

Image
Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli 1-1. Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza. Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari. Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.

David Ferrer amemchapa Alexandr Dolgopolov na kufanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Swedish Open.

Image
David Ferrer amemchapa Alexandr Dolgopolov na kufanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Swedish Open. Hili ni kombe kubwa kwa Muispaniola huyo tokea ameshinda kikombe cha Vienna Open miaka miwili iliyopita. Ferrer ameshinda kwa seti 6-4 6-4 na kupata taji la 27 kwenye historia yake katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali. Ferrer anashika nafasi ya 46 kwa ubora duniani.

Mlinzi muIsrael amempiga risasi na kumuua mshambuliaji raia wa Jordan ambaye alimvamia karibu na ubalozi wa Israel nchini Jordan.

Image
Mtu mwingine raia wa Jordan naye aliuwawa wakati wa ufyatuaji risasi kwa mujibu wa Israel. Mlinzi huyo aliripotiwa kujeruhiwa. Mshambuliaji alikuwa ni seremala aliyekuwa akifanya kazi katika jengo uliko ubalozi wa Israel. Hiki ni moja ya visa vibaya zaidi kati ya nchi hizo tangu zisaini mkataba wa mani mwaka 1994. Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem Polisi wawili wa Israel wauawa Jerusalem Israel kujenga nyumba 560 mashariki mwa Jerusalem Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho. Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman. Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.

Muumini wa kanisa la katoliki Adrian Mpanda amefariki baada ya kupigwa risasi mbili akiwa anasubiri kuingia kwenye ibada katika kanisa la parokia ya kibangu wilaya ya ubungo jijini Dar es salaam

Image
Muumini wa kanisa Katoliki, Adrian Mpande amepigwa risasi mbili akiwa anasubiri kuingia  kanisani katika Parokia ya Kibangu wilaya Ubungo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa George Ng’atigwa ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa Mpande alikuwa akisubiri kuingia kanisani majira ya saa tatu asubuhi lakini alikuja mtu mmoja aliyekuwa anatembea kwa miguu na kumpiga risasi ubavuni na mkononi, hali iliyosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Alisema kuwa mtu huyo alikimbia lakini watu waliokuwa maeneo hayo walifanikiwa kumkamata baada ya kuishiwa risasi wakati akijaribu kuwatishia. Aliongeza kuwa baada ya kumkamata mtu huyo, waliwasiliana na jeshi la polisi ambalo lilifika na kuondoka naye kwa ajili ya taratibu za kisheria na kwamba majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika zahanati iliyokuwa karibu. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tuki...