Posts

Showing posts from July, 2017

Yaliyo jili magazetini hii leo tarehe 25/7/2017

Image

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake.

Image
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana alisomewa mashtaka ya uchochezi na kurudishwa rumande akisubiri hatma ya dhamana yake. Lissu alisomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Serikali, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbert Mashauri. Mawakili watano wa upande wa Jamhuri waloshiriki katika kesi hiyo, waliiambia Mahakama kuwa Lissu alitenda kosa hilo la jinai Julai 17 mwaka huu katika eneo la Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Lissu ambaye alikuwa akitetewa na jopo la mawakili 20 wakiongozwa na Fatma Karume, alikana mashtaka dhidi yake. Mbunge huyo pia alisikika akisema, “kwakweli halijawahi kuwa kosa la jinai.” Baada ya kusikiliza pande zote mbili Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi Julai 27 ambapo hatma ya dhamana ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) itakapojulikana.

Shirika la TRA imeipelekea madai yake katika kampuni yam Acacia imeiambia kuwa wanadaiwa kodi ya kwanzia mwaka 2000 hadi 2017 hadi 2017 na pangea inadaiwa kodi ya kati ya mwaka 2007 hadi 2017 yenye dhamani ya shilingiTrilioni 425 .......

Image
Kampuni ya Acacia imeeleza kuwa imepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inayoonyesha kuwa migodi yake ya Bulyanhulu inadaiwa kodi ya kati ya mwaka 2000 hadi 2017 na Pangea inadaiwa kodi ya kati ya 2007-2017. Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya Acacia jana Julai 24, imeeleza kuwa taarifa hiyo imetokana na ripoti za kamati mbili za Rais zilizoonyesha kuwa wamekuwa hawatangazi kiasi halisi cha mapato yao wakisafirisha mchanga kwenda nje ya nchi. Acacia wamesema kuwa, bado wanaendelea na msimamo wao wa kupinga matokeo ya kamati hizo na kusema kuwa wamekuwa wakitangaza mapato yao.  Aidha, wameeleza kwamba bado hawajapata nakala za ripoti za kamati ya kwanza na ya pili zilizowasilishwa kwa Rais Magufuli Mei 24 na Juni 12 mwaka huu. Uchambuzi uliofanywa na TRA umeonyesha kuwa Mgodi wa Bulyanhulu unadaiwa na serikali takribani Tsh 344.8 trilioni (USD 154bn) na Mgodi wa Pangea takribani Tsh 76.1 trilioni (USD 36bn). Uchambuzi huo una...

Hatimae real Madrid ya fungwa na Manchester united kwa mikwaju ya penati na kumaliza dakika 90 sare ya magoli 1-1...........

Image
Manchester United wameifunga Real Madrid kwa mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa sare ya goli 1-1. Anthony Martial alitumia juhudi binafsi na kumtengenezea pande Jesse Lingard na kuandika goli la kwanza. Casemiro aliisawazishia Madrid kwa njia ya penalti baada ya mlinzi mpya wa United Victor Lindelof kumuangusha Theo Hernandez katika eneo la hatari. Penalti saba kati ya kumi hazikuingia nyavuni.

David Ferrer amemchapa Alexandr Dolgopolov na kufanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Swedish Open.

Image
David Ferrer amemchapa Alexandr Dolgopolov na kufanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Swedish Open. Hili ni kombe kubwa kwa Muispaniola huyo tokea ameshinda kikombe cha Vienna Open miaka miwili iliyopita. Ferrer ameshinda kwa seti 6-4 6-4 na kupata taji la 27 kwenye historia yake katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali. Ferrer anashika nafasi ya 46 kwa ubora duniani.

Mlinzi muIsrael amempiga risasi na kumuua mshambuliaji raia wa Jordan ambaye alimvamia karibu na ubalozi wa Israel nchini Jordan.

Image
Mtu mwingine raia wa Jordan naye aliuwawa wakati wa ufyatuaji risasi kwa mujibu wa Israel. Mlinzi huyo aliripotiwa kujeruhiwa. Mshambuliaji alikuwa ni seremala aliyekuwa akifanya kazi katika jengo uliko ubalozi wa Israel. Hiki ni moja ya visa vibaya zaidi kati ya nchi hizo tangu zisaini mkataba wa mani mwaka 1994. Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem Polisi wawili wa Israel wauawa Jerusalem Israel kujenga nyumba 560 mashariki mwa Jerusalem Mamlaka za Israel hazijazungumzia kisa hicho. Ubalozi huo wenye ulinzi mkali uko mtaa wa Rabiyeh ambalo ambao ni wa kifahari mjini Amman. Siku ya Ijumaa maelfu ya watu waliandamaa mjini Amman kupinga hatua ya Israeal ya kuweka vifaa vya kutambua chuma katika aneo takatifu kwa waislamu na wakiristo mashariki mwa Jerusalem.

Muumini wa kanisa la katoliki Adrian Mpanda amefariki baada ya kupigwa risasi mbili akiwa anasubiri kuingia kwenye ibada katika kanisa la parokia ya kibangu wilaya ya ubungo jijini Dar es salaam

Image
Muumini wa kanisa Katoliki, Adrian Mpande amepigwa risasi mbili akiwa anasubiri kuingia  kanisani katika Parokia ya Kibangu wilaya Ubungo jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa George Ng’atigwa ambaye ni shuhuda wa tukio hilo amesema kuwa Mpande alikuwa akisubiri kuingia kanisani majira ya saa tatu asubuhi lakini alikuja mtu mmoja aliyekuwa anatembea kwa miguu na kumpiga risasi ubavuni na mkononi, hali iliyosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Alisema kuwa mtu huyo alikimbia lakini watu waliokuwa maeneo hayo walifanikiwa kumkamata baada ya kuishiwa risasi wakati akijaribu kuwatishia. Aliongeza kuwa baada ya kumkamata mtu huyo, waliwasiliana na jeshi la polisi ambalo lilifika na kuondoka naye kwa ajili ya taratibu za kisheria na kwamba majeruhi alikimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kupatiwa huduma ya kwanza katika zahanati iliyokuwa karibu. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Suzan Kaganda alithibitisha kutokea kwa tuki...

Hatimae mwalimu atupwa mbaroni kwa kufanya mapenzi na mwanafunzi wake

Image
Mwalimu  wa somo la Baiolojia katika shule ya sekondari ya wasichana ya St Therese  ambaye alidakwa akifanya mapenzi na mwanafunzi katika maabara ya shule hiyo amesimamishwa kazi akisubiri hatua za kinidhamu dhidi yake. Ofisa Elimu wa Wilaya, Christopher Sinkamba akizungumza alisema kwamba maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya wananchi wengi kulalamika.  Sinkamba alisema mwalimu anayehusika ametambuliwa kama Raphael Mwape na kwamba sasa anasubiri hatua za kinidhamu dhidi yake. Alisema kwamba utawala wa shule ulifikisha suala hilo Polisi lakini walishindwa kumshtaki kwa tuhuma za kubaka kwa kuwa binti huyo ni zaidi ya miaka 16.  Na wakati alipoulizwa swali kwanini mwanafunzi huyo wa kike ametimuliwa shule, ofisa huyo alisema kwamba hawajamfukuza lakini walilazimika kumhamisha shule kutokana na sheria za shule hiyo. Ilielezwa kuwa tukio hilo lilifanyika saa 12 jioni ambapo Mwape alionwa na mabinti wengine wawili wa shule hiyo akifanya mapenzi na bi...

KIUNGO Mzimbabwe Thabani Scara Kamusoko ambaye Jumatano iiliyopita aliongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga baada ya mavutano na uongozi kwa takribani mwezi mmoja, ameanza balaa lake mazoezini.

Image
KIUNGO Mzimbabwe Thabani Scara Kamusoko ambaye Jumatano iiliyopita aliongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga baada ya mavutano na uongozi kwa takribani mwezi mmoja, ameanza balaa lake mazoezini.  Baada ya kusaini mkataba huo mpya utakaomfanya adumu Jangwani hadi Julai 2019, Kamusoko alijiunga na mwenzake kwa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya. Mchezaji huyo mtaalamu wa kugawa pasi alisajiliwa Yanga SC mwaka 2015 kutoka FC Platinums ya kwao Donald Ngoma ambaye naye tayari ameongeza mkataba Jangwani.  Kamusoko pamoja na wachezaji wenzake walifanya mazoezi ya kupasha na kunyoosha viungo baada ya hapo waliingia kwenye hatua nyingine ya kukimbia katika mashine maalum na kunyakua vitu ili kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao.  Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh alisema kwa mijubu wa ratiba ya kocha wataendelea na mazoezi ya gym hadi mwishoni mwa wiki hii ili kuwaweka sawa wachezaji wao kabla ya kuanza rasmi harakati za kujenga ki...

Hatimae kocha wa Liverpool Jurgen klopp ametishia kupitisha panga kwenye timu yangu

Image
KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ametishia kutembeza panga kwenye safu yake ya ushambuliaji endapo msimu ujao watashindwa kuonyesha makali yao.  Hadi sasa kocha huyo ameshaongeza nguvu kwenye safu hiyo kwa kuwasajili Mohammed Salah kutoka AC Roma na huku tayari Dominic Solanke vilevile akiwa ameshawasili.

Hatimae taifa star kutolewa na Ruwanda leo

Image
Atimae timu ya tanzania  kucheza na  Ruwanda   leo kule nchini ruwanda katika wanja wa  Nyamirambo kule ruwanda  katika timu ya  tanzania  ikiongonzwa na  wachezaji kama John Bocco Rhaeli Manula Kichuya Mao Mzamiru Saimoni Msuva Michaeli  Nyoni Bonifa Mpaka  dakika ya tisini mpira kuisha  hakuna mtu aliyeiyona  goli la mwenzie mpaka dakika zimekusha   kwa matokeo hayo yameifanya ttimu ya tanzania  kuanga mashondano kwa siku ya leo taifa star  italejea nyumbani kujianda kwa michezo ambayo inakalibia kuanza

Hatimae simba kusajili kiungo kipya kutoka Ghana taarifa zilizopo ni kwamba amepeleka kwa kambini afrika kusini

Image
KLABU ya soka ya Simba ni kama imenogewa na wanandinga wa kutoka nchini Ghana ambapo sasa imeshusha straika mwingine na taarifa zilizopo ni kwamba amepelekwa kambini nchini afrika kusini. Wachezaji wa wekundu hao kwa sasa wapo nchini Afrika Kusini kwa kambi ya siku 20 ya kujiandaa na Ligi Kuu sambamba na ile tamasha la kila mwaka la Simba Day linalofanyika kila ifikapo Agosti 8. Taarifa za ndani zinazohusiana na masuala ya usajili zinasema kuwa raia huyo wa Ghana ni Thomas Agyei ambaye ni mpachika mabao ambaye Simba iliripotiwa kumtuma mjumbe mmoja kwenda kumalizana nae huko kwao.  Agyei ambaye pia ni mchezaji kijana ameripotiwa kukamilisha hatua muhimu za kujiunga na kikosi cha Mnyama msimu huu ambapo mara baada ya kutaarifiwa ujio wake amekuwa akisubiliwa kwa hamu. Habari ambazo bado ni motomoto zinasema kuwa kocha Joseph Omog ameridhishwa na kiwango chake kupitia CD ya aina ya uchezaji wake na ameuagiza uongozi ufanye hima kumpandisha pipa ili kuwahi kambi ya Sa...

Real Madrid imemwingiza mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcus Rashford kwenye mipango yao ya usajili ya kiangazi hiki.

Image
Real Madrid imemwingiza mshambuliaji kinda wa Manchester United Marcus Rashford kwenye mipango yao ya usajili ya kiangazi hiki. Mabingwa hao wa Hispania wataamua kumfungia kazi Rashford iwapo watakutana na ugumu wa kumsajili kinda wa Monaco Kylian Mbappe . 

MCHEZAJI wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva sasa yuko tayari kwenda kuanza maisha mapya ya soka la kulipwa nje ya Tanzania na hii ikiwa ni mara yake ya kwanza. “Kila kitu kipo tayari, naondoka wakati wowote kuanzia leo (jana).

Image
MCHEZAJI wa klabu ya Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, Simon Msuva sasa yuko tayari kwenda kuanza maisha mapya ya soka la kulipwa nje ya Tanzania na hii ikiwa ni mara yake ya kwanza. “Kila kitu kipo tayari, naondoka wakati wowote kuanzia leo (jana). ” “Nitaelekea Morocco kujiunga na klabu ya Difaa Al Jadida ambao ni washindi wa pili Ligi Kuu Morocco. Naondoka Yanga SC, timu uliyonilea na kunipa mafanikio.” Msuva ameongeza kwa kusema: “siondoko kwa ubaya ndio maana nimefuata taratibu zote ambapo viongozi wote wa pande mbili wameafikiana na kufanya biashara, naamini iko siku nitarudi kuitumikia Yanga tena, ila mpaka nitimize malengo yangu ya kucheza soka la kulipwa Ulaya na kuwa miongoni mwa wanasoka waliofanikiwa nchini.”  “Bada ya Morocco Mungu akijaalia basi nitakuwa Ureno, lakini hasa ni Hispania maana nina uwezo wa kucheza la Liga.” Mchezaji huyo amemalizia kwa kuwashukuru wana Yanga kwa ushirikiano mkubwa waliompatia, anaamini kupitia kipaji chake, iko furaha amewap...

Hatimae timu ya mbeya city imesema itatumia jezi mpya kuwa ni kiingilio uwanjani katika mchezo wa kirafiki dhidi ya azam fc unaotarajiwa kuchezwa jumapili hii . jijini mbeya

Image
KLABU ya Mbeya City imesema itatumia jezi mpya kuwa ni kiingilio uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Jumapili hii jijini Mbeya. Ofisa habari wa Mbeya City, Shaa Mjanja alisema kuwa mchezo huo umeandaliwa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara itakayoanza Agosti 26, mwaka huu.  Alisema, mchezo huo utamsaidia kocha wao, Kinah Phiri kuweza kutambua makosa ya kiufundi kwa wachezaji na kuyasawazisha mapema kabla ya msimu mpya. Hivyo kwenye mchezo huu wa kirafiki klabu imeona kutumia jezi mpya na bidhaa mbalimbali kama vile skafu kuwa kiingilio uwanjani,” alisema. Alisema tayari klabu hiyo kupitia wakala maalum imeingiza sokoni jezi na bidhaa muhimu, lengo likiwa ni kuwarahisishia mashabiki na wadau kupata bidhaa hizo. “Siku hiyo mashabiki na wadau wa soka jijini Mbeya watalazimika kuingia uwanjani kwa tiketi ya jezi au bidhaa yoyote ya klabu ya Mbeya City,” alisema.  

Taifa star na timu ya ruanda wanacheza siku ya leo mpaka

Image
SHIRIKISHO la mpira wa miguu Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” na Taifa Stars ya Tanzania kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN).  Stars na Rwanda zinarudiana leo Jumamosi kwenye uwanja wa Nyamilambo mjini Kigali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Mwanza wiki iliyopita na timu inayoshinda ndio itakayofanikiwa kusonga mbele.  Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utachezwa saa 10:00 jioni kwa saa za Rwanda ambazo ni sawa na 9:00 alasiri kwa saa za Tanzania na utachezeshwa na Brian Nsubuga Miilo ambaye ni raia wa Uganda atakayepuliza kipyenga cha kati.  Atasaidiana na Ronald Katenya (Line 1), pamoja na Dick Okello (Line 2), wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Cheleneti Ally Sabila hukukamishina wa mchezo atakuwa ni Ally Ahmed Mohammed kutoka Somalia.  Stars ina matumaini ya kuso...

Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.

Image
Wakili wa Tundu Lissu, Fatma Karume amesema polisi walikataa kumpa dhamana mteja wake jana jioni mara baada ya kukamatwa akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere. Karume amesema baada ya kufikishwa polisi, Lissu alitakiwa kuandika maelezo na kupewa onyo kwa kosa la uchochezi. “Lakini cha ajabu mpaka sasa hivi hatujaambiwa Lissu kamchochea nani, kosa la uchochezi lazima lilete madhara au uhalifu kwa wengine na ni lazima liwe la uhalifu.” Amesema Amesema hata walipouliza nani anayeweza kuruhusu mteja wake apate dhamana hiyo waliambiwa imezuiwa kwa amri kutoka juu. Lissu ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) alikuwa akielekea Kigali, Rwanda, katika mkutano wa wanasheria wa Afrika. Karume amesema uchochezi lazima liwe ni jambo la uhalifu na mpaka sasa polisi hawajamwambia Lissu aina hiyo ya uchochezi. “Hili ni jambo la kisiasa, Lissu amezuiwa kwenda kwenye mkutano wa wanasheria wa Afrika, jambo hilo linawafanya hata wanasheria wote wa Afrika...

Trump legal team spokesman Mark Corallo resigns, reports say

Image
The spokesman for US President Donald Trump's personal legal team has resigned, media reports say. Mark Corallo was a spokesman for Marc Kasowitz, who is defending Mr Trump in an inquiry into alleged Russian meddling in last year's election. Reports said that Mr Corallo disagreed with the alleged strategy of Mr Trump's lawyers to discredit or limit the team directing the investigation. There has been no comment from him or the Trump team. Mr Corallo is close to Justice Department special counsel  Robert Mueller , who is leading the Russia investigation, and has praised him publicly,  Politico website reports. He had grown frustrated with the operation of the legal team and the warring factions and lawyers, the report adds. Russia: The 'cloud' over Trump How did we get here? How Trump team's story changed Mr Mueller  has hired big names  to join his team, which is also investigating whether there was any collusion with the Trump team, which bo...

Vumbi kutoka mwenzini launzwa dola milioni 1.8 mjini New York

Image
Mfuko moja uliotumika na mwananga Neil Amstrong kukusanya violezi vya mwezi umeuzwa kwa dola milioni 1.8 mjini New York. Mfuko huo kutoka kwa chombo cha angani Apolo 11 mwaka 1969 ulinunuliwa katika eneo la Sotheyby na mtu asiyejulikana. Mfuko huo bado una vumbi na mawe madogo madogo kutoka mwezini. Mnada huo unajiri baada ya mapambano mahakamani kuhusu umiliki wa kifaa hicho cha kipekee kutoka kwa ujumbe wa Apollo 11 ambao ulikuwa katika mikono ya mtu binafsi. Baada ya chombo hicho cha angani kurudi duniani, vifaa vyote vilipelekwa katika jumba la makumbusho la Smithsonian. Hatahivyo mfuko huo uliwachwa katika boksi katika kituo cha vyombo vya angani cha Johnson kutokana na makosa ya kihesabu. Baadaye haukutambulika wakati wa mnada wa serikali, ukiuzwa kwa dola 995 pekee kwa wakili mmoja wa Illinois 2015. hatahivyo mamlaka inayosimamia vyombo vya angani Nasa ilijarabu kuuchukua mfuko huo, lakini mapema mwaka huu jaji mmoja aliamuru kwamba ulimilikiwa na mnunuzi huyo...

Manchester United imejipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester City katika debi ya kwanza ugenini huku ziara za 2017 zinazofadhiliwa na Aon zikiendelea kuipatia ushindi the red Devils.

Image
Manchester United imejipatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wapinzani wao wa jadi Manchester City katika debi ya kwanza ugenini huku ziara za 2017 zinazofadhiliwa na Aon zikiendelea kuipatia ushindi the red Devils. Romelu Lukaku na Marcus Rashford waliisaidia United katika mabao yote mawili yaliofungwa katika kipindi cha kwanza. Kikosi hicho cha Jose Mourinho kilianza kwa mashambulizi huku Anders Herrera akianzisha juhudi hizo mapema, huku mashambulio mengine yakitoka nje ya eneo la hatari ,United wakimjaribu kipa mpya wa City Ederson. David De Gea alilazimika kuwa macho katika upande mwengine huku Raheem Sterling akishambulia mara mbili , kabla ya Chris Smalling kuzuia mashambulizi mawili yaliofanywa na Patrick Roberts na Sterling. United hatahivyo ilifanikiwa dakika nane kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza baada ya Lukaku kupata pasi muruwa kutoka kwa Paul Pogba na kucheka na wavu. Dakika mbili baadaye Marcus Rashford aliifungia United bao la pili akifunga baada ya...