Posts

Showing posts from June, 2017

Kauli za mawakili baada ya Malinzi na Mwesigwa kunyimwa dhamana

Image
Baada ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwanyima dhamana Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na afisa wa fedha Nsiande Mwanga, jopo la mawakili wa utetezi wameonekana kutoridhika na wateja wao kukosa dhamana. “Washtakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani halafu wanaomba tena upelelezi wa kesi wakati suala tayari lipo mahakamani hiyo ndio pointi kubwa ambayo tumeiibua halafu kitu kingine tulichokiibua ni pamoja na maombi ya dhamana,”  Jarome Msemwa-wakili upande wa utetezi. “Tumeiomba mahaka itoe dhamana kwa wateja wetu, kuna sheria ya Bunge inayokataza dhamana halafu kuna katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu dhamana. Kwa hiyo kwa amri ya mahakama ambayo imesomwa leo (jana) wateja wetu wanapelekwa rumande hadi Jumatatu Julai 3, 2017.” “Sikutarajia katika muda na wakati kama huu kutakuwa na mashitaka yanayowakabili yanayofika 28 ya aina ileile lakini ndani yake yanatengenezwa machache kufanywa ya tutakatisha fedha wakati mas...

Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz

Image
STAA wa muziki wa kizazi kipya, Q Chillah ametambulisha wimbo mpya alioshirikishwa na rapa Chid Benz kwa staili ya kumwaga machozi wakati akiwa kwenye mahojiano. Q Chillah alisema kwamba anaguswa na hali ya Chid Benz ambaye alikaa kwenye rehab kwa muda mrefu akitibu tatizo la matumizi ya dawa za kulevya. “Nimeguswa na hali ya Chid Benz na najua nimepitia hali nyingi sana kwenye maisha ambazo Chid pia amepita,” alisema rapa huyo . “Lakini kikubwa kilichoniliza nimewahi kuwapoteza marafiki wakubwa sana ambao niliwapenda, wasanii wenye majina makubwa Tanzania, mtu kama Albert Mangweha “Ngawair” Mwana hiphop ambaye mimi sijawahi kumuona zaidi yake,” alimaliza rapa huyo. Marapa hao Q Chillah na Chid Benz kwa wakati tofauti wote waliwahi kukiri kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu MKuu wa TFF Selestine Mwesigwa watafikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 29, 2017 kwa ajili ya taratibu za kimahakama kuchukua nafasi yake.

Image
Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu MKuu wa TFF Selestine Mwesigwa watafikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Juni 29, 2017 kwa ajili ya taratibu za kimahakama kuchukua nafasi yake. Afisa uhusiano wa TAKUKURU Musa Misalaba amethibisha kwamba, Malinzi na mwenzake watafikishwa mahakama ya Kisutu leo. Malinzi na Mwesigwa wanashikiliwa na TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano lakini tangu kushikiliwa kwao, TAKUKURU hawajaweka wazi sababu za kuwashikilia licha ya kusema wanawahoji na kuendelea na uchunguzi wao.

Bunge limetenga chumba maalum kwa ajili ya wabunge wenye watoto wachanga kunyonyesha watoto wao wakati vipindi vya bunge vinaendelea.

Image
Bunge limetenga chumba maalum kwa ajili ya wabunge wenye watoto wachanga kunyonyesha watoto wao wakati vipindi vya bunge vinaendelea. Uamuzi huo umetangazwa leo (Jumatano) bungeni na Naibu Spika Dk Tulia Ackson mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni. "Ofisi ya Bunge inataarifu kuwa imetenga chumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea kwa wabunge wenye watoto wachanga,"amesema. Amewasihi wabunge wenye watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao angalau miaka miwili kama inavyoshauriwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao.

Image
Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao.  Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao. Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria. Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika. Wengine ni aliyekuwa katibu mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka (FAT sasa TFF), Michael Wambura na mjumbe wa ...

Wanaharakati katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na maandishi ya amri 10 za Mungu

Image
Wanaharakati katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na maandishi ya amri 10 za Mungu, kwenye uwanja wa makao makuu ya bunge la jimbo hilo. Wanasiasa walipitisha kauli ya ujenzi wa mnara huo wa jiwe wenye urefu wa futi sita, katika eneo la Little Rock mnamo mwaka wa 2015. Muungano wa haki na uhuru wa raia nchini Marekani ACLU, umewasilisha kesi mahakamani kutaka kuondolewa mara moja kwa mnara huo, ukisema kuwa unaleta mgawanyiko na unakiuka ahadi ya uhuru wa kidini kwa wote, katika katiba ya Marekani. Seneta wa chama tawala cha Republican, Jayson Rapert, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa kutaka kuwekwa kwa jiwe hilo , alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na msimamo wa mahakama kuu ya Marekani, na hivyo ni jambo zuri kwa jimbo la Arkansas.

KITENDO cha mashabiki wa klabu ya Yanga kuichoma jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa inavaliwa na kiungo Haruna Niyonzima, kimezidi kupondwa na wanamichezo wengi.

Image
KITENDO cha mashabiki wa klabu ya Yanga kuichoma jezi namba 8 iliyokuwa inavaliwa inavaliwa na kiungo Haruna Niyonzima, kimezidi kupondwa na wanamichezo wengi.  Afisa habari na Mawasiliano wa Simba anayeitumikia adhabu ya kufuingiwa kujishughulisha na soka, Haji Manara amesema kwamba kitendo kinachofanywa na washabiki wa Yanga sio cha kistaarabu.  Manara ameandika katika ukurasa wake wa Instagram akisema kwamba katika miaka ya karibu wachezaji kadhaa wa Simba wamekuwa wamehimaiaYanga, lakini Simba hawajawai kuchoma jezi zao.  “Wenzetu ustaarabu wao ni ziro, iliwajiandae kuchoma nyengine hivi kalibuni,” amesema Manara katika ukurasa wake huo. Manara amesema kwamba wanachofanya Yanga nao wasione ubaya kufanyiwa, akimaanisha kwamba ya Yanga kuwasajili wachezaji wa Simba.  Awali, katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alilani hatua hiyo ya washabiki wa timu yake kuichoma moto jezi hiyo, na kufananisha na upuuzi na kukosa kupevuka kisoka.  “ku...

Ramadhani Chombo aliyekuwa kiungo wa Mbeya City amesema hivi sasa yuko huru akisubiri timu inayoeleweka ili aweze kujiunga nayo

Image
ALIYEKUWA kiungo wa Mbeya City, Ramadhani Chombo “Redondo” amesema kuwa hivi sasa yuko huru akisubiri timu inayoeleweka ili aweze kujiunga nayo msimu ujao.  Kiungo huyo ambaye aliwahi kutiomkia Denmark wakati akiwa kwenye kituo cha Dyoc, amesema kuwa kuna timu zinamnyemelea lakini bado hawajafikia makubaliano.  “Nipo huru hivi sasa, bado hakuna timu tuliyofikia makubaliano kwa ajili ya msimu ujao. Nasubiri kuona nini kitaendelea,” alisema Redondo.  “Nipo kwenye mapumziko ya muda mfupi kabla ya kujua wapi nitaelekea msimu ujao, nitaweka wazi nikishafikai makubaliano na sehemu nitakayoenda,” alimaliza. Ramadhani Redondo aliwahi kuitumikia klabu ya Simba kabla ya kutimkia Mbeya City.

Atimae Haruna nyionzima kujiunga na simba kuanzia msimu ujao

Image
KITENDO cha Haruna Niyonzima "Fabregas" kujiunga na Simba na kuanza kuitumikia kuanzia msimu ujao, maana yake itakuwa ametimiza amza yake ya siku nyingi ambayo anadaiwa kuwa alikuwa nayo. Imedaiwa kuwa kiungo huyo nyota wa kimataifa raia wa Rwanda alikuwa na hamu ya kujiunga na Simba siku nyingi, lakini pia hata viongozi wa Simba wakati huo walikuwa wanatamani kumsajili. Aliyekuwa mwenyekiti wake, alitamani kumsajili Niyonzima. Mzee dalali walimuhoji akasema kwamba kama kweli viongozi sasa wa Simba watamsajili fundi huyo wa mpira wa miguu basi Simba kuna habari kwamba asilimia 90 wameshamalizana na Niyonzima na kwamba kinachosubiriwa sasa ni mkataba wake na Yanga kumalizika ili atambulishwe. Mzee Dalali amesema kwamba Niyonzima ni kati ya viongozi bora Afrika, hivyo anaamini kama akitua kuichezea Simba, basi msimu ujao wa Ligi Kuu Bara watakuwa na kikosi imara. Mwenyekiti huyo wa zamani wa Simba amesema kwamba kwa muda mrefu amekuwa akifurahishwa na uwezo wa Haruna, hasa uw...

Atimaye Deus Kaseke anatarajia kuongeza mkataba wa miaka miwili kutumikia klabu ya Yanga

Image
KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Deus Kaseke anatarajia kuongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo iliyobeba ubingwa wa Ligi Kuu bara kwa mara tatu mfululizo.  Kaseke aliyekuwa likizo kwao Mbeya, alirejea Dar es Salaam kuja kumalizana na uongozi wa Yanga baada ya kuwekewa mezani mkataba wa miaka miwili.  “Hakuna sehemu yoyote nitakayosaini zaidi ya Yanga ambao nimemalizana nao katika kila kitu muhimu,” alisema kiungo huyo.  “Yanga ni nyumbani, hizo taarifa za mimi kujiunga na Singida United nazisikia tu lakini ukweli ni kuwa ninasaini Yanga,” aliongeza. Dues Kaseke amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha George Lwandamina tangu alipotua akitokea timu ya Mbeya City.

Atimae klabu ya as kigali Rwanda imeiomba Simba kumuuzia mshambuliaji wake Laudit Mavugo

Image
KLABU ya AS Kigali Rwanda imeomba Simba kumuuzia mshambuliaji wake Laudit Mavugo ambaye aliwahi kuitumikia klabu hiyo.  Habari ambazo sarianews  inazo zinasema kwamba klabu hiyo imetuma maombi Simba kutaka kuhuzwa  nyota huyo raia wa Burundi.  Mtandao mmoja umeandika juzi kwamba Mavugo alikuwa amesafiri hadi jijini Kigali kufanya mazungumzo na klabu yake hiyo ya zamani na kwamba alikuwa amekubali kusaini tena mkataba wa miaka miwili kwa dau ambalo halijawekwa wazi.  Hata hivyo, Simba kupitia kwa makamu wake wa rais, Geoffrey Nyange Kaburu imesema kwamba Mavugo amekuwa na wasiwasi baada ya kumsajili John Bocco Adebayor, Emmanual Okwi na mpango wa kumsajili Donald Ngoma, huenda akakosa namba katika kikosi hicho.  Lakini Kaburu amesema kwamba Mavugo bado ni mchezaji wao na ana mkataba wa msimu mmoja zaidi kuendelea kufanya kazi Msimbazi.  “Mavugo ana mkataba na klabu na bado klabu haijapokea ofa yoyote kutoka popote ikimuitaji ...

Hatimaye Simba kukamilisha usajili wa kiungo wa yanga Haruna Niyonzima

Image
Baada ya timu ya Simba kukamilisha usajili wa kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima usajili ambao ulikuwa unaogelewa sana na wapenzi wa Soka hapa nchi, taarifa mpya ni kwamba kiungo huyo atapewa jezi namba 8. Kiungo huyo machachari ameacha na Yanga baada ya kucheza misimu sita mfululizo na amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya zaidi ya milioni 100 za Kitanzania. Habari kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa, Haruna atapewa jezi hiyo iliyokuwa ikitumiwa na Mwinyi Kazimoto. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kazimoto hayupo kwenye mipango ya mwalimu kwa msimu ujao baada ya mkataba wake kumalizika. Haruna ambae ni kipenzi cha wana Yanga, atatumbulishwa rasmi na timu yake mpya katika sherehe za Simba Day Agosti, mwaka huu.

imebaki siku moja kufika siku ya jumatano kwa kuwasili straika Donald ngoma akisubiriwa nchini akitokea kwao Zimbabwe

Image
WAKATI kesho Jumatano straika, Donald Ngoma akisubiriwa kutua nchini akitokea kwao Zimbabwe, tayari uongozi wa Simba umeshamuwekea mezani mkataba wa miaka miwili. Ngoma ambaye msimu uliopita alikuwa akiitumikia Yanga ambayo tayari amemaliza mkataba, msimu ujao anaweza kuvaa jezi za Simba kutokana na timu hiyo kuonesha nia ya dhati ya kuihitaji saini yake. Mzimbabwe huyo aliyejiunga na Yanga misimu miwili iliyopita, tayari ameshafanya mazungumzo ya awali na Simba huku ikitaarifiwa kwamba yamekwenda vizuri. Chanzo cha ndani ya Simba, iliambia sarianews  kuwa baada ya kuwa na asilimia kubwa ya kumnasa Ngoma, tayari wameshaandaa mkataba ili akitua tu asaini. “Ni kweli Ngoma tunamuhitaji na tayari tumeshaongea nae kila kitu kimekwenda sawa, alisema atawasili baada ya kumalizika kwa Sikukuu ya Idd,”kilisema chanzo hicho.

Aisha Manula amesha jiandaa kuachana na timu yake ya Azam FC na kujiunga na timu ya mara baada ya mkataba wake kukamilisha alieleza jana

Image
Golikipa wa Azam FC Aishi Manula amesema ameshajiandaa kiakili kuachana na klabu yake ya sasa na kwenda katika klabu yake mpya mara baada ya mkataba wake kumalizika. “Kumekuwa na maswali mengi kwamba kwa nini umekwenda Simba kwa sababu wanaamini hivi vilabu vikubwa vinaharibu viwango vya wachezaji na wachezaji wengi ambao wameenda huko huwa wanapatwa na mataizo hasa ya mikataba na kutopewa mishahara.” “Niwahakikishie, mimi nakwenda kujiunga na moja ya hivyo vilabu nikiwa najua hayo yote. Kiujumla nimejiandaa na hayo yote yatakayotokea nimeshajiandaa nayo kwa hiyo nakwenda sehemu ambayo najua tayari kwamba kuna matatizo ya kucheleweshewa mishahara.” “Watu wa nje ambao hawajui wanaamini Azam kuna maisha mazuri na hawajui hali halisi ambayo ipo ndani ya Azam, wote tulikuwa Azam na maisha ya pale tunayajua. Mimi siyo mpumbavu wa kiasi hicho kuondoka Azam huku nikiwa najua sehemu ambayo kilakitu kipopo halafu naenda sehemu ambayo vitu hivyo havipo.” “Wanatakiwa waelewe mimi kama mchezaj...

Makaburi kumi yagundurika katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo katika mkowa wa kasai

Image
Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inasema kwamba imepata zaidi ya makaburi kumi ya pamoja katika mkoa wa Kasai, mahali ambapo vikosi vya serikali na makundi ya waasi yametuhumiwa kwa mauaji ya raia. Mwendesha mastaka wa kijeshi Generali Joseph Ponde amesema anaamini mauaji hayo yamefanywa na sehemu waasi wa Kamuina Nsapu ambao wamekuwa wakipiga vita majeshi ya serikali. UN yathibitisha makaburi ya pamoja DRC Zaidi ya watu 500 wauawa DRC tokea mwezi Machi Zaidi ya watu 3000 wameuwawa DRC tangu Oktoba Mnamo wiki iliyopita Umoja wa Mataifa ulielezea hofu yake juu ya mauaji yanayoendelea kila uchao katika mkoa huo, ambapo takriban watu elfu mbili waliangamizwa katika kipindi cha miezi mitatu. Umoja huo aidha ulinyooshea kidole jeshi la taifa la Kongo kwa kutekeleza uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu. Hata hivyo jopo maalum la uchunguzi wa mauaji hayo iliamua kwamba hakuna uhalifu wowote wa kivitu uliyotekelezwa na kwamba hakuna mapigano yaliyotangazwa rasmi mkoani Kasa...

Watu 6 wafa maji na wengine 16 hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama maji inchini colombia

Image
Idara ya polisi nchini Colombia, imesema kuwa yamkini watu 6 wamefariki ika ajali ya kuzama kwa boti moja la abiria katika bwawa moja, katika mji mmoja ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Watu 16 hawajulikani waliko, baada chombo cha ghorofa nne, lilipoanza kujaa maji mara tu lilipo n`goa nanga katika ziwa moja la kujiundia, karibu na mkahawa mmoja maarufu kwa watalii la Guatapé, kilomita 45 mashariki mwa Medelini, siku ya Jumapili. Kulikuwa na watu 150 ndani ya chombo hicho. Maandamano nchini Colombia Kwa mjibu wa mtu mmoja aliyeshuhudia ajali hiyo, Juan Quiroz, ameiambia BBC kuwa, chombo hicho kilichukua chini ya dakika 5 kuzama. Maboti mengine madogo madogo yalifika kwa kasi na kuanza kuwaokoa watu kutoka majini na orofa ya juu ya chombo hicho. Aidha, ndege za helikopta na wapiga mbizi wa kijeshi wameonekana mahali pa mkasa huo wakijaribu kuwaokoa manusura. Mapigano kusitishwa rasmi Jumatatu Colombia Hakujatolewa taarifa zaidi ya kilichosababisha chombo hicho cha majini ku...

Onyo limetolewa kwa yeyote atakaye mpinga Rais John Pombe Magufuli kwa atakaye mrudisha mtoto aliye pewa mimba shuleni taharifa hii imetolewa na Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amezionya taasisi zisizo za Serikali zinazohamasisha kudai haki ya mtoto anayepata mimba kurejeshwa shuleni kuacha mara moja na zikiendelea atazifutia usajili. Mwigulu ameyasema hayo leo, Jumapili wakati alipomwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Parokia ya Kisasa Mjini hapa. Amesema Serikali haitaomba ushauri wala maoni kwa sababu maelezo yaliyotolewa na Rais, John Magufuli ni maagizo ya Serikali. Waziri huyo amesema Serikali imetoa haki ya kila mtoto kupata elimu kwa kuifanya kuwa bure kwa hiyo atakayeikosa asitafute kisingizio. "Rais ametoa haki hiyo sasa hivi elimu ni bure, halipi tuition wala nini, atakayeamua kuachana na haki hiyo asitafute kisingizio, asipeleke lawama kwa Serikali, "amesema.

TID atishia kwenda kituo cha kati

Image
Mwimbaji TID aka Mnyama kama anavyopenda kuitwa, ametishia kutinga katika kituo cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Quick Rocka na kundi la OMG. TID ambaye ana historia ya kufikishwa yeye kwenye kituo ha polisi na hata kufungwa miezi kadhaa, sasa amebadili upepo na yeye anahitaji haki yake kisheria. Kupitia mtandao wa Instagram, Mnyama ametishia kufika polisi kuwasilisha malalamiko yake kutokana na kile alichodai kundi la OMG na Bosi wao Quick wametumia wimbo wake ‘Watasema’ bila ruhusa yake. Hivyo, anahitaji kulipwa angalau milioni 20 kama kifuta jasho kwa kazi yake iliyowahi kushinda tuzo mbili. “Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema, ameandia msanii huyo. Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal ...

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger

Image
Arsene Wenger amemuorodhesha winga wa Manchester United Anthony Martial katika orodha yake ya washambuliaji anaotaka kuwanunua kiangazi hiki.  Kocha huyo wa Arsenal ameanza kumkatia tamaa kinda wa Monaco Kylian Mbappe na sasa anampigia hesabu Martial.  Wenger anajiandaa kulipa pauni milioni 40 kwa Martial, ambaye amekosa nafasi ya kudumu Old Trafford chini ya Jose Mourinho.  Hata hivyo Wenger anahofia kuwa Mourinho anaweza kumbania kutokana na uhasimu mkubwa ulioko kati yake na kocha huyo wa Manchester United.

Vicent Bossou amesema kwamba yuko tayari kurudi kwenye kikisi cha Yanga ikiwa viongozi wa klabu hiyo watamwita

Image
BEKI wa kati, Vicent Bossou amesema kwamba yuko tayari kurejea kwenye kikosi cha Yanga ikiwa tu viongozi wa klabu hiyo watamwita na kukaa meza moja ya mazungumzo.  Bossou ambaye kwa hivi sasa yuko nchini Togo kwa ajili ya mapumziko mafupi, alisema kwamba mpaka sasa hajawasiliana na viongozi kuhusiana na suala lake la mkataba mpya lakini atakuwa tayari endapo ataitwa.  “Hakuna mawasiliano yoyote ambayo yamefanyika mpaka wakati huu, lakini klabu ya Yanga naipa kipaumbele zaidi na nipo tayari kurejea endapo nitaitwa wakati wowote kuanzia sasa  alisema beki huyo''.  Nipo mapumziko hivi sasa baada ya kuisha kwa mzunguuko wa Ligi na hakuna timu ambayo nimefanya nayo mazungumzo kwa ajili ya kujiunga nayo,” aliongeza.  Beki huyo ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa ambao wamemaliza mikataba ndani ya klabu ya Yanga ambayo kwa hivi sasa inafanyia kazi maoni yaliyoachwa na kocha George Lwandamina juu ya wachezaji inayowahitaji.

Kiwanya cha Garden Breeze cha Magomeni jijini Dar es salaam kitajazwa watu siku ya Idd Mosi

Image
BENDI ya African Minofu imejinasibu kukijaza kiwanja cha Garden Breeze, Magomeni, Dar es Salaam kwa mashabiki wengi zaidi siku ya Idd Mosi pale watakapoporomosha burudani ya kukata na shoka.  Bosi wa African Minofu, Matei Joseph aliiambia sarianews  kuwa, anaamini muziki watakaouporomosha utakuwa mkubwa kiasi cha kuchangia kukifanya kiwanja hicho kujaa mashabiki watakaovutwa na burudani yao.  “Binafsi, ni msanii wa siku nyingi ninayefahamu mbinu nyingi za kimuziki, hasa katika kuwavuta mashabiki, hivyo naahidi kukijaza kiwanja hicho kwa muziki mnene zaidi,” amesema Matei.  Matei amesema kuwa, shoo yao ya Idd Mosi katika kiwanja hicho imepangwa kuanza kurindima majira ya saa 12:30 jioni na kuendelea hadi majogoo, ambapo watatumbuiza vibao vyao vipya pamoja na vile vya zamani.  Amesema kuwa pia watarindimisha nyimbo mbalimbali za kukopi kutoka mataifa mbalimbali, huku wakiahidi kuyapa kipaumbele maombi ya mashabiki pamoja na wapenz...

kuna kila dalili simba kuwa moto wakuotea mbali baada wakitaka kumsajili mchezaji kutoka zambia

Image
KUNA kila dalili kikosi cha Simba msimu ujao kikawa moto wa kuoteambali, has baada ya kuripotiwa kutaka kumnasa kiungo fundi mithili ya Haruna Moshi “Boban”, Michael Chaila raia wa Zambia.  Inasemekana Chaila ana uwezo mkubwa wa kusimama juu na mipango hiyo ya kumleta Msimbazi inafanywa kwa siri ili isije kuharibika, Chaila ni mchezaji wa Zesco United ya Zambia, timu ambayo alikuwa akichezea straika mwingine wa Simba, Juma Luizio “Ndanda. ” Inasemekana kiungo huyo mwembamba ana mashuti makali na mwepesi kubadili mchezo, kwa watu wanaomfahamu wanasema Chaila ni zaidi ya Niyonzima na ujio wake unakuja baada ya dili ya kumpata Niyonzima kukamilika.  Simba bado inaendelea kufanya usajili ukiwa na maana ya kukiboresha kikosi chake ambacho msimu ujao kitashiriki michuano ya kimataifa na tayari wameshasajili wachezaji sita wapya ambapo inajiandaa kutambulisha wengine.  Waliosajiliwa na Simba hadi sasa ni Jamal Mwambeleko, Yusuph mlipili, John Bocco, Shomary Kap...

Atimae uwanja wa mkwakwani Tanga wafanyiwa marekebisho

Image
UWANJA wa Mkwakwani jijini Tanga unatarajiwa kufanyiwa marekebisho kwenye baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua zilizokuwa zikinyesha sehemu mbalimbali hapa nchini.  Akiongea na sarianews, meneja wa uwanja huo, Nassor Makau amesema ukarabati huo umelenga maandalizi mapya ya Ligi ya Mkoa ambayo yamepangwa kufanyika uwanjani hapo.  “Kama unavyojua, hivi sasa tuko kwenye maandalizi ya Ligi ya mkoa wa tanga, hivyo tunatakiwa kukarabati maeneo ya uwanja, hasa eneo la ardhi kwa lengo la kuuweka kwenye hali nzuri ya kuchezewa,” alisema Makau.  Alisema, wataendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha uwanja huo unakarabatiwa kila wakati ili kutumiwa na klabu zinazoshiriki Ligi mbalimbali, ikiwemo ile ya daraja la kwanza.

Mwanasheria mkuu TBS ahukumiwa miaka mitano jela au faini ya Milioni 13.9

Image
Baada ya kuachiwa huru siku ya Jumatano na kukamatwa tena, jana aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Bitaho (54) amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni 13.9 au kifungo jela miaka mitano baada ya kusomewa upya mashtaka na kukiri. Bitaho alifikishwa tena katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana asubuhi na kusomewa mashitaka nane likiwemo la kufanya kazi nchini bila kibali na kutoa taarifa za uongo. Bitaho ambaye ni Raia wa Burundi, alifutiwa mashtaka yake, na baadae kukamatwa, alisomewa hukumu hiyo, na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa. Akisoma hukumu hiyo Nongwa alisema kuwa mahakama imesikiliza maombi ya pande zote mbili na kwamba katika kosa la kwanza hadi la saba mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh laki tano au kifungo jela kuanzia miaka miwili hadi mitatu na kwamba kosa la nane mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 10 au kifungo jela miaka mitano. Alisema, kwa taratibu zilizopo, baada ya mshitakiwa kukutwa na hatia anatak...

vijana wakimtukuza mungu katika tamasha la vijana arusha katika ukumbi wa ajtc

Image
vijana wakimtukuza mungu leo katika viwanja vya ajtc arusha hamakweli  watu wamebarikiwa  na kumtukuza mungu.waimbaji  tofauti tofauti wakimtukuza mungu  na watu waliweza kufunguliwa  shida zao  na atimae aliye fungwa na vifungo na shetani vilifunguka na watu waliweza kumtukuza mungu kwa  roho na kweli . watu wakiwa katika uwepo wa bwana wakisikiliza na kutafakari maajabu ya  mungu  aliyo yatenda katika maisha yao hapa duniani   waumini wote wametakiwa kumuabudu muhumba wao katika maisha yao wanapo ishi duniani  wamkumbuke muhumba wao popote walipo wakumbuke kwamba hapa duniani si kwao bali sisi ni watu tunao pita hatuna makao bali kwetu ni mbinguni alipo baba  muhumba bingu huyo ni mwalimu  Elihuluma stanford chao akimuinuwa mungu  katika viwanja vya ajtc leo  alimtukuza  mungu kwa jitiada zake  zote kwa kadri mungu alivyo mjalia aliweza kumuhinuwa mungu.hakika mungu...

hatimaye mchezaji bora wa hispania Lioneil Messi pamoja na baba yake waponea chupuchupu kuingia jela wafanikiwa kuikwepa jela

Image
Almanusra mshambuliaji wa klabu ya Barcelona Lioneil Messi na baba yake waende jela baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya ukwepaji kulipa kodi. Mwezi July mwaka jana Lioneil Messi na baba yake walikutwa na hatia katika kesi hiyo iliyokuwa ikiwakabili na baada ya hukumu waliamriwa kulipa faini au kutumikia kifungo. Messi na baba yake walihukumiwa kifungo cha miaka 21 japokuwa kifungo hicho kilikuwa cha nje ya gereza kwa kuwa ilikuwa ni chini ya miaka miwili. Messi na baba yake waliajiri kundi la mawakili ambao walijaribu kuwatete katika kesi hiyo bila mafanikio na baadae mamlaka za kisheria zikawahukumu. Sasa taarifa zinasema Lioneil Messi amekubali kulipa faini ya euro 252,000 na baba yake akilipa euro 180,000 na hiyo itawafanya kuepuka kifungo kilichokuwa kinawakabili. Huu ni muendelezo wa makosa ya ukwepaji kodi nchini Hispania ambapo Cristiano Ronaldo na kocha Jose Mourinho nao wapo katika uchunguzi wa kesi kama ya Messi na baba yake.

kongamano la vijana wakimsifu kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni

Image
leo tarehe  23/6/2017 wakimsifu mungu  katika viwanja vya AJTC  waimbaji mbalimbali wamehudhuria katika tamasha hilo akiwemo muhimbaji Elihuruma Stanford Chao kutoka arusha ,Emanuel  kutoka ajtc Arusha ,pamoja na kwaya ya preas  kutoka ajtc arusha vijana wakimsifu Mungu kwa roho na kweli katika viwanja vya Ajtc       watu wakiimba wimbo wa kuabudu   hakika bwana ameonekana mahali hapa  Godfreay  akiwaongoza  wenzake katika  ukumbi wa ajtc leo  vijana wakimuhabudu muhumba wao katika viwanja vya  ajtc siku ya leo ijumaa tulivu ya tarehe 23/6/2017 vijana wakimtukuza bwana kwaro  na ukweli katika viwanja vya Ajtc leo  mapema