Maduka ya muda’ na umuhimu wake kibiashara

WAJASIRIAMALI zaidi ya 40 walikusanyika nyumbani kwa Balozi wa Italia nchini, jijini Dar es Salaam. Ulikuwa mkusanyiko uliolenga kuuza bidhaa mbalimbali kwa mfumo ambao unatajwa ni wa ‘maduka ya chap chap’.
Mjasiriamali katika sekta ya ubunifu wa mavazi, Mustafa Hassanali ndiye aliyeratibu tukio hilo la kibishara lililohusisha zaidi wajasiriamali ambao ni wabunifu wa bidhaa mbalimbali za Kitanzania. Eneo la wazi la nyumbani kwa balozi huyo, zikaonekana bidhaa mbalimbali zilizo kwenye mpangilio mzuri.
Inawezekana tafsiri ikajielekeza kulinganisha tukio hilo na gulio. Lakini kwa aliyebahatika kufika na kujionea, atabaini ni tofauti na magulio ya kawaida hasa kutokana na namna ya uendeshwaji wake. Wakati kwenye magulio imezoeleka kuona wauzaji wakiwa wamepanga bidhaa holela, kwa maduka hayo ya muda mfupi, bidhaa zilipangiliwa kwa umakini.
Baadhi ya bidhaa ziliwekwa juu ya meza na nyingine (hususani nguo) zikining’inizwa kwa kutumia vifaa maalumu. Eneo hilo la maduka, lilitawaliwa pia na vionjo vya burudani ya muziki ikiwaburudisha watu waliofika kwa ajili ya manunuzi.
Pia kulikuwa na mighahawa yenye chakula chenye mvuto. Hassanali katika kuzungumzia zaidi uamuzi wa kuandaa tukio hilo, anasema ni baada ya kugundua kuwa ni njia rahisi ya kuwakutanisha wajasiriamali wakanadi bidhaa na pia wakawa na wigo mkubwa zaidi katika biashara zao.
Anasema alibaini kuwa wananchi na hasa katika mazingira ya mjini ambao wanakosa muda wa kutosha wa kufanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali dukani. “Kwa njia hii, wamesogezewa huduma,” anasema.
Anasema wanaouza vito, mavazi, viatu, herein, marashi, saa na huduma nyingine zinazosimama katika dhima nzima ya urembo, ndio walengwa wakubwa. Mjasiriamali, Irene Rwakatale ni miongoni mwa walioshiriki katika tukio hilo.
Irene ambaye anajihusisha na uuzaji wa mavazi ya kibunifu ya wanawake ambayo huyabuni mwenyewe, anasema mkusanyiko huo umemsaidia kukutana na wateja wakiwamo ambao hawakufahamu kazi zake.
Anasema, licha ya walionunua bidhaa zake moja kwa moja, wengine wameonesha shauku ya kupata bidhaa zake. Anasema, imekuwa pia ni nafasi kwake kukutana na wajasiramali wengine ambao wamebadilishana mawazo na kibiashara ikiwa ni pamoja na kupeana mbinu mpya.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger