Sports Extra Ndondo Cup 2017 mambo yameiva, kaa mkao wa kula

Wakati hatua ya awali ya michuano ya Sports Extra Ndondo Cup 2017 ikielekea ukingoni, kuelekea draw ya hatua ya makundi, kila kitu kitakuwa live au sikuhizi tunasema mubashara.
Zoezi la kuchezeshwa draw kwa ajili ya kupata makundi nane (8) litafanyika siku ya Alhamini kupitia Clouds TV na channel nyingine ambazo zitatangazwa kadiri muda unavyozidi kwenda.
Ukiachilia mbali draw kuonekana live kwenye TV, zitatangazwa pia radio ambazo unaweza ukafatilia mchakato mzima wa upangaji wa makundi. Wataalam wa masuala ya technology wanaendelea kupambana kuhakikisha kuna kuwa na website ya Ndondo Cup, social media za Ndondo Cup na platform nyingine kulingana na itakavyo wezekana.
Kutakuwa na makundi nane yenye timu nne kwa kila kundi, kutakuwa na timu nane ambazo zitakuwa zinaongoza makundi hayo timu hizi (nane) ni zile ambazo msimu uliopita zilikata tiketi ya kuingia hatua ya robo fainali (kwa hiyo timu zote zilizofanikiwa kuingia hatua ya robo fainali msimu uliopita ndio zitakuwa vinara wa makundi na kila timu itakuwa na kundi lake).
Halafu timu zilizotolewa katika hatua ya 16 bora ni timu nane nyingine ambazo zenyewe zitakuwa kwenye bakuli la pili wakati bakuli la tatu na la nne ni timu 16 za mwaka huu ambazo zimefanikiwa kufuzu hatua ya makundi.

Comments

Popular posts from this blog

Siku ya jana yalifanyika maombi na mazishi mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki Alhamisi asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam picha na sauti 5 bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

Atimae Anthony Martian aongezwa katika orodha ya kusajiliwa katika msimu huu katika club ya Manchester United taharifa hiyo imetolewa na Arsene Wenger

Atimae Singida United kuanza maandalizi yake kuelekea msimu mpya wa ligi kuu tanzania bara